Sambaza....

Mshambuliajiwa timu ya soka ya Barcelona Lionel Messi amesema kutupwa katika nafasi ya tanokwenye tuzo za mchezaji bora za Ballon d’Or siku ya Jumatatu iliyopita sio sababu ya kujituma na kufunga mabao mawilidhidi ya RCD Espanyol usiku wa jana.

Messia ambaye alifunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 4-0 kwenye dabi ya Cataluña amesema kiwango alichokionesha kwenye mchezo huo hakina uhusiano wowote wakudhihirisha ubora wake baada ya kutupwa nje ya tatu bora ya tuzo za Ballon d’Orkwa mara ya kwanza baada ya miaka kumi.

“Hapana”Messi alijibu alipoulizwa kama kiwango chake kimechangiwa na kutokuwepo kwenye nafasi tatu za juu za Ballon d’Or, “Wote tulikuwa na motisha toka mwanzo wa mchezo, tukiwa na hamu ya ushindi, tulijua lazima tuwe hivyo kwa sababu tupo nyumbani, lakini pia kutokana na ubora wa wapinzani wetu ambao wamekuwa na msimu mzurihadi sasa,” amesema.

Messikatika mchezo huo alifunga mabao mawili kwa njia ya Free Kick na kutoa assist kwa Ousmane Dembele wakati bao lingine likifungwa na Luis Suarez licha ya mara kadhaa Messi kukosa mabao ya wazi kuweza kuiongezea unene akaunti yake ya mabao.

Kwa ushindi huo Barcelona wanafikisha alama 31 na kujikita kileleni kwa tofauti yaalama 3 na anayeshika nafasi ya pili (Sevilla) na alama nane dhidi ya wapinzani wao wakubwa Real Madrid ambao jioni hii wanashuka dimbani kuumana na SD Huesca.

Sambaza....