Kocha Mkwasa
Blog

Mkwasa afukuzwa Yanga !

Sambaza....

Kocha wa Yanga, Luc Eymael
amemuondoa kikosini msaidizi wake,
Boniface Mkwasa na kocha wa
makipa, Peter Manyika wakati
wakijiandaa kuikabili Mtibwa jioni
ya jana mjini Morogoro.

Luc Eymael licha ya kutoweka wazi
sababu alitamka jana wakati anazungumza na waandishi wa habari kuwa .
“Mimi ni Kocha mwenye weledi.Nimewaacha na kwenda na kocha wa timu ya U-20, Saidi Maulid ‘SMG’.“Ni vigumu kuzungumzia hilo
pamoja na ukweli kuwa kuna
makocha hawajasafiri nasi, mechi
lazima ichezwe na nina kocha
msaidizi ambaye ndiye kocha mkuu
wa timu ya U-20, Maulidi”

Luc Aymael kocha mkuu wa Yanga sc.

“Kazi itafanyika pamoja na kuwa na kikosi finyu chenye majeruhi na
wagonjwa,” alisema Eymael, ambaye
habari za ndani zinasema
amewakataa makocha hao na
anataka kuwa na benchi jipya
kabisa.

Ukiachana na Mapinduzi Balama
ambaye amevunjika mguu, wachezaji
wengine, Papy Tshishimbi, Haruna
Niyonzima na kipa Farouk Shikhalo
ni majeruhi huku Patrick Sibomana
akimuuguza mkewe.

Benchi la ufundi la Yanga!

Hata hivyo, alisema amemwambia
Metacha amfuate Morogoro ili
kuongeza nguvu kama tu atakuwa
amepata nafuu.

“Metacha ni mgonjwa na hataweza
kucheza mechi kutokana na hali yake
kwa sasa.Alilazwa na kutolewa,
amekuja huku kuongeza morali, ila
kipa namba tatu, Ramadhan Kabwili
na kipa wa timu ya U-20, Geofrey
watakuwepo katika mechi hiyo,”
alisema Eymael, ambaye baadhi ya
viongozi wa Yanga walidokeza jana
kwamba, siku zake klabuni hapo
zinahesabika.

Sambaza....