ASFC

Mtibwa sugar yabomoa Stand ya Shinyanga

Sambaza....

Timu ya soka ya Mtibwa sugar ya Turiani Manungu mkoani Morogoro, imefanikiwa kuingia fainali ya kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kuwachapa wenyeji Stand United kwa mabao 2-0 mchezo uliopigwa kunako dimba la CCM Kambarage mkoani Shinyanga

Shujaa wa Mtibwa sugar hii leo, ni kiungo wa zamani wa vilabu vya Ruvu shooting na Yanga sc Hassan Dilunga aliyefunga mabao hayo katika dakika za 29 na 38, za kipindi cha kwanza na kuifanya Mtibwa kutinga fainali ikiwa ni mara yake ya kwanza katika michuano hiyo

 

Mtibwa sugar, inayonolewa na mchezaji wake wa zamani Zuber Katwila, sasa itakutana na mshindi wa nusu fainali nyingine inayotaraji kupigwa Jumatatu kunako dimba la Namfua kati ya wenyeji Singida United wakiikaribisha Jkt Tanzania ya Dar es salaam

Fainali ya michuano itafanyika Juni 2, 2018 kunako dimba la kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid mjini Arusha, na bingwa wa michuano atapata kitita cha Tsh milioni 50, pia akiwakilisha Tanzania kunako michuano ya kombe la shirikisho Afrika

Mshindi wa pili atapata Tsh miliini 10, huku mchezaji bora akipata Tsh milioni 1 sawa na kipa bora, mfungaji bora huku mchezaji bora wa mchezo wa fainali akizawadiwa Tsh 500,000

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x