Hassan Mwakinyo
Stori

Mwakinyo Kuwania Ubingwa wa WBO nchini kwa mara ya kwanza

Sambaza....

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo anatarajia kupanda ulingoni kuwania mkanda wa Dunia wa WBO chini ya Kampuni ya Promosheni ya ngumi za kulipwa nchini PAF Promotion Entertainment Company LTD katika pambano litakalopigwa Agosti mwaka huu.

Akizungumza mbele ya Waandishi wa habari promota kutoka PAF, Hassan Mwakinyo alisema kuwa kwa sasa amejipanga kuhakikisha anakata kiu ya Watanzania katika mchezo wa ngumi za kulipwa kwa kucheza pambano ambalo la mkanda ambao hajauwahi kuchezwa nchini.

“Baada ya kukosekana uliongoni katika ngumi za ushindani Hassan Mwakinyo kwa muda mrefu nawashukuru ndugu zangu waandishi kwa kuja hapa natarajia kupanda ulingoni mwezi ujao katika pambano kubwa la kuwania mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBO.

“Muda mrefu nilikua natamani nipate pambano kama hili lakini nilikua bado sina vigezo, sasa nashukuru nimevipata na utakua wakati mzuru sana kwangu kupata pambano hili. Ningefurahi pia kwa mabondia wa Tanzania wangepata nawao nafasi kama hii tena wakipigana hapahapa nchini lakini bado vigezo hawana.”

Mwakinyo aliongeza kuwa: “Ukimya wangu haukuwa wa bure, nitakidhi kiu ya mashabiki wangu ambao hawajaniona muda mrefu ulingoni. Nitawastarehesha na  kuwaburudisha mashabiki wangu. Nimejiandaa na bado najiandaa vyema mpaka sasa kwa pambano hilo.”

“Kwa Tanzania boxer yoyote anayetaka kupigana namimi kwanza agombe mkanda huu ninaokwenda kuupigania. Lakini pia hata mabondia wakubwa huwa wanacheza sparling hivyo kama kuna bondia anataka hivyo aje Masaki tupigane.” alisema Mwakinyo.

Sambaza....