Blog

Naipenda Yanga – MWINYI ZAHERA

Sambaza....

Jana Yanga walimfukuza kazi kocha wao mkuu , Luc Eymael. Baada ya Luc Eymael kufukuzwa maneno yamekuwa mengi kuhusiana na kocha ambaye anatajwa kwa ajili ya kuchukua nafasi yake.

Yanatajwa majina mengi kuja kuchukua nafasi ya Mbelgiji huyo.  Kocha wa zamani wa Simba , Patrick Aussems anatajwa kwenye orodha hiyo . Pia kwenye orodha hiyo kuna makocha wawili wa zamani wa Yanga , Mwinyi Zahera na Hans Van Pljuimn.

Baada ya taarifa hizi kuzagaa mtandao huu umenasa mazungumzo ya aliyewahi kuwa mkuu wa Yanga , Mwinyi Zahera akijibu tetesi hizi. Kocha huyo amedai kuwa yeye anaipenda Yanga kutoka moyoni na yuko tayari kurudi Yanga.

“Mimi naipenda Yanga na niko tayari kurudi Yanga kuifundisha kwa sababu naipenda kutoka moyoni” – alisema kocha huyo mwenye maneno mengi. Swali moja linabaki kwa wana Yanga , wako tayari kumkaribisha tena Mwinyi Zahera kwa mara ya pili ?


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.