Blog

Nantes watozwa faini kwa kuomboleza kupotea kwa Emiliano Sala.

Sambaza....

Klabu ya soka ya Nantes ya nchini Ufaransa imepigwa faini kwa kosa la kuwasha mioto wakati wakiombeleza kupotea kwa mshambuliaji wao Emilliano Sala mwezi uliopita.

Shirikisho la sok nchini Ufaransa limeitoza klabu hiyo faini ya shilingi milioni 43.7 baada ya mashabiki wake kuwasha baruti na mioto katikati ya bango kubwa lilibeba picha ya mshambuliaji huyo wakiombeleza siku chache baada ya kupotea angani akiwa anaelekea nchini Uingereza.

Sala aliichezea Nantes mechi 133 na kufanikiwa kufunga mabao 48 jambo ambalo liliwashawishi mabosi wa Cardiff city kumsajili lakini kwa bahati mbaya hakufanikiwa kucheza hata mchezo mmoja kwani alipata ajali ya ndege na kufariki akitokea kuwaaga wachezaji wenzake wa Nantes.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.