Blog

NENDA BALINYA,MIMI NGOJA NIENDELEE KUANGALIA HII FILAMU.

Sambaza....

 

NA Mustafa Mtupa.

Nikiwa ndani ya Dala dala ya mbagala ikiwa inelekea maeneo ya Makumbusho huku watu wakiwa wamejaa hadi dirishani.

Nilimsikia Mzee mmoja wa makamo akinong’ona kwa sauti ya chini saana akisema.”ndani yatimu yetu ya yanga kwa jinsi hali ilivyo mbaya kila mmoja anamuhisi mwenzake mchawi”

Nikiwa nimetega sikio na kusikia maneno hayo.halmashauri ya ubongo wangu ikaniletea Faili la mtazamo ambalo baada ya kulifungua nikakutana na waraka uliokuwa umeandikwa kwa maandishi meusi ambao ulikuwa ukisomeka kama ifuatavyo.

Ni kweli yanga inapitia nyakati ngumu kifedha japo kuna wadhamini wa kutosha.hii inatokana na mfumo mbovu walio jiwekea.

Hali ya matokeo yasiyo ridhisha na muenendo mbaya wa Timu wakati wa Kocha Zahera ulianza kufanya kauli ya Mzee yule ianze kuishi kwenye nembo ya klabu ya yanga.

Wakati ule hawa kuhangaika saaana kumtafuta mchawi kwani walikuwa na Zahera ambaye kwa hulka yake wana Yanga karibia woote alishawatoka maabani hivyo kazi ya kumbatiza Mwinyi zahera uchawi haikuwa na changamoto kubwa.

Baada ya Zahera kuondokaa kiti chake amekaimu Mkwasa ambaye ni kipenzi cha Wanachama walio wengi wa klabu ya Yanga.Mtu ambaye ni Mgumu kumbatiza Jina la mchawi wa Yanga na kumuonesha kidole kuwa yeye ndio anaifanya yanga iwe na mwenendo mbaya.

Badala yake Cheo hicho cha uchawi wa Klabu yanga hivi sasa kinatafuta wa kukivaa. Baada ya Jumba bovu kukwepa vikali tena kwa staili ya mfumo. Wa 4.4.2 na Mwenyekiti wa klabu hiyo.shida ikahamia kwa Juma Balinya pamoja na Sadney Urikhob ambao ni miongoni mwa Watu waliovikwa kitambaa hicho hali ya kuwa hakiwahusu kabisa.

Balinya (Kulia)

Kinacho endelea kwenye Klabu ya Yanga kwa sasa ni sawa na Mpita Njia kuangukiwa na Jumba bovu tu wakati mwenye nyumba ni mwengine.

Kwa mtazamo wangu matatizo yanayo tokea yanga yali tengenezwa mda sana japo Matokeo yake ndiyo tunayaona sasa ivi.shida ni kuwa viongozi walio ichukua timu wamekutana na Bahari ya matatizo wakati uwezo wao wa kuogelea ni kwenye mto.

Hii muvi ya kumsaka mchawi bado natumai kuiona inaendelea.huku bila ya kujua kwamba anaye mtafuta mchawi naye ni mchawi.

Naomba nifunge faili hili kwa kusema kuwa shida ya Yanga sio Wachezaji wala kocha ila hawa ambao wana wamiliki Wachezaji wanawatumia hawa Wachezaji ili kuficha ukweli kwamba wanaogopa kuogelea kwenye Bahari wakati wamezoea kuogelea kwenye mito.

Kalamu nyeusi
@insta,MtotoWamkulima99
@facebook:Mustafa Abainder

0687058966

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.