Mataifa Afrika

Nguema aondolewa kwenye kikosi cha Taifa.

Sambaza....

Beki wa kati Gilchrist Nguema ameenguliwa katika kikosi cha timu ya Taifa cha Gabon kinachojiandaa na mchezo wake wa mwisho wa kufuzu kwenye fainali za Mataifa Afrika (AFCON) dhidi ya Burundi.

Nguema ambaye alikuwa miongoni mwa wachezaji 23 walioitwa kujiandaa na mchezo huo wa Machi 23, 2019 mjini Bujumbura, ameondolewa kwenye kikosi hicho na kocha Daniel Cousin baada ya shirikisho la soka la Gabon (Feagafoot) kubaini kwamba beki huyo hana timu kwa sasa.

“Baada ya uchuguzi wa kina, imebainika kwamba Nguema ambaye kwa sasa anaishi nchini Gabon hana timu yoyote kwa miezi sasa, na timu ya Taifa sio sehemu ya majaribio,” imesema sehemu ya taarifa ya Fegafoot.

Nafasi ya Nguema ambaye awali alikuwa akiichezea Macau Benifica ya nchini Macau imezibwa na beki Farnk Obambou anayekipiga kwenye timu ya soka ya Al Ittihad ya nchini Libya.

“Rais wa Fegafoot anaendelea kuwakumbusha makocha mbalimbali wa timu za taifa, kwamba wanaowajibu wa kuwateua wachezaji ambao wapo katika hali nzuri ili kuimarisha dhana ya uwajibikaji, kujituma na heshima kwa shirikisho letu,” imesema taarifa ya Fegafoot.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.