Blog

Nimetosha kucheza Afrika – Simon Msuva

Sambaza....

Wakati Ibrahim Ajib akikataa ofa ya kwenda TP Mazembe , Simon Msuva ana mawazo tofauti kabisa kuhusiana na maisha yake ya mpira wa miguu.

Mchezaji huyo wa zamani wa Yanga, amedai kuwa kwa sasa imetosha kwake yeye kuendelea kucheza Afrika na anatafuta changamoto mpya.

Simon Msuva

“Ninachoweza kusema ni kwamba dili langu limefikia hatua nzuri, nitaweka wazi kila kitu mambo yakikamilika.

Sipendi kusema nitaenda sehemu gani afu muda utakapofika unachokitegemea kikaenda hovyo.

Ila wanaonipenda wazidi kuniombea ili kila kitu kiende kama kilivyopangwa, nadhani imetosha kucheza Afrika, nawaza kukutana na changamoto nyingine mpya za soka kwingine”-Alisema Simon Msuva


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.