David Molinga "Falcao"
Blog

Njaa yawakimbiza kina BALINYA, MOLINGA Yanga !

Sambaza....

  1. Mabingwa wa kihistoria nchini Dar Young African (Yanga) inakumbana na changamoto kubwa kwa sasa ndani ya klabu hiyo Baada ya baadhi ya wachezaji nyota wa klabu hiyo kudaiwa kuvunja mkataba na klabu hiyo kwa Madai ya kutolipwa mshahara wao kwa muda wa miezi mitatu.

Kwa mujibu mwa taarifa kutoka chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya klabu hiyo ya Yanga kimeelezea kuwa wachezaji hao ambao wengi wao ni wa nje ya nchi wameshawasilisha barua ya kuvunja mkataba ndani ya Yanga na nakala nyingine wakiwa wamezipeleka FIFA.

Wachezaji ambao wanadaiwa kuvunja mkataba na klabu hiyo ya Kariakoo ni pamoja na Issa Birigimana, Sadney , Kalengo, Juma Balinya , Lamine Moro na David Molinga.

Jana mwenyekiti wa klabu hiyo Dkt. Mshindo Msola alidhibitisha kuwa klabu hiyo iko kwenye ukata mkubwa kwa sasa, Kwani viongozi wapya walikuta madeni makubwa sana , madeni ambayo ndiyo wanayashughulikia kwa sasa.

Mwenyekiti huyo alidai kuwa wameachana na mshambuliaji wao Sadney Baada ya kutoridhishwa na kiwango chake na Leo kumetoka taarifa ya kuachana na Juma Balinya ambaye alisajiliwa kutoka klabu ya Polisi ya nchini Uganda.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.