Blog

Ole Gunnar Solskajer, Wewe ni nani haswa?

Sambaza kwa marafiki....

Ulimuona Ole Sosopi Sululu (Ole Solskajer) The Great White Maasai dakika ile baada ya United yake kupoteza kwa Magoli mawili kwa sifuri Magoli ya Kylian Mbappe na Presnel Kimpembe? Uliona namna alivyojibu swali la kwamba mshatolewa? Alisema “United haijatolewa Ni ngumu kwenda Robo lakini Hatushindwi United imeshafanya haya mara nyingi sana lakini ukiangalia Uwezo wetu tukicheza nje ya Nyumbani kila mtu anatufahamu Uwezo wetu kwa sasa, Tuna Imani kubwa” alimaliza Ole.

Jana niliulizwa swali na Jamaa zangu sehemu huko nilisema Niko very Optimistic United tunasonga kwenda Quarter Final ya CL, mimi ni nani hata niwe na Mashaka wakati Manager kashasema ana Uhakika wa kugeuza Matokeo? Wakati naangalia Mechi jana kuanzia Team Selection hadi Squad Depth nilisema ni rahisi sana kushinda ile mechi ya jana kuliko mechi nyingine yoyote ile, kwa kukukumbuka Maneno ya Ole!

Gunnar akimpongeza Rashford

Nilitoa Sababu za Kiufundi kwa Jamaa aliyeniuliza swali nilimwambia Kocha wa PSG Tomas Tuchel ana wakati mgumu sana kuliko mechi ya kwanza, nikaendelea leo anakuja Akiwa Blind yaani hajui United ipi inakuja kucheza nae kwasababu wachezaji 10 likely wa kikosi cha kuanza wapo Majeruhi unakuja na Game plan ipi? Nikaendelea kwa kusema Mechi ya pale OT ilikuwa Rahisi sana kwa Tuchel kwasababu alicheza kwenye Mpango wa United kwa ku deal na watu kama Paul Pogba ambae kwa siku za Karibuni ndio amekuwa Focal point ya Mashambulizi na upatikanaji wa Magoli wa United! Sikuliona hili likitokea dhidi ya timu ambayo haijui plan yake ya mechi, wakati huo huo Ole ameshaangalia Mpango wao kwenye mechi ya Awali na namna wanacheza mechi nyingine!

Katika ku Cement (Kukazia) maneno yangu nikamkumbusha jamaa maneno ya Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp alipomaliza Mechi vs United alisema ….”Tulijiandaa kucheza na Kikosi cha kwanza cha United, majeruhi ya United yalituharibia na kutufanya kushindwa kushinda” kiushabiki unaweza kuibeza kauli hii ila kwenye Mbinu ambazo timu huwa inajiandaa Makocha siku zote huwa wanafanya Mazoezi kuelekea aina ya Mpinzani wanaeenda kukabiliana nae na hapa ndipo Klopp alifeli kwasababu hakuwa na mpango B wa kukabiliana na Opponent ambae anakuja na wachezaji asiowajua wanacheza vipi?

Mwisho nikawakumbusha Kituko kimoja Wakati yupo LvG kwenye Helm tukijiandaa kuelekea game vs Chelsea wiki nzima Bwana Mkalimani Hozee Dad Mlishi alimuandaa Kurt Zouma ku deal na Fellaini wakati wanaingia Wachezaji wa United na Wawakilishi wao akaonekana pacha wake Fellaini Jukwaani pale Darajani Kocha Msaidizi wa Mou akajua LvG amekuja na Mkakati mpya na kumwambia Boss wake Fellaini hayupo maana ndugu yake huyo Fellaini wanafanana sana na wote wanaweka “Mawigi” kwenye vichwa vyao! Hapa maana yake nini kama ingekuwa hivyo yule Kurt Zouma asingekuwa na la kufanya pale Uwanjani! Maana aliletwa kwa kazi ya Kumzuia Fellaini ambae hayupo angemzui nani? Angekuwa additional to requirements tu!

So sikuwa na shida juu ya matokeo ya jana kwa United kuishtua Dunia hapa nilikuwa nina Uhakika ila Namna ile plan ya Ole ilivyofanya kazi kama alivyosema hapo ndipo ninajiuliza Ole Wewe ni nani haswa? Ole alisema Tutaingia kutafuta Goli la kwanza then tutatafuta la pili then tutamantain game hadi dakika 10 za Mwisho then tutaangalia namna ya kumaliza Mechi na kila kitu kikawa katika Mpango! Najiuliza Ole wewe ni nani? Namna ulivyoitoa Chelsea pale Stamford Bridge, namna ulivyoibutua Arse888 pale Uwanja wa Ndege, namna ulivyowarudishia Form yao Paul Pesa Mbili Madafu Labile Pogba, David “Spiderman” De Gea, Victor “Iceman” Lindelof, Marcus Rashford, Jesse “Messi” Lingard na kwa sasa Hii form ya Romelu Bolingoli “Omushambuliaji” Lukaku naomba nikuulize hivi wewe ni nani Haswa?

Ole kwa Hiki unachoendelea kukifanya hapa viunga vyetu vya Trafford na huko Upenuni kwao kuna watu wanasonya huko na kununa lakini wewe Jamaa yaani kila sifa upewayo unasema sio ya kwako ni Wachezaji ndio wanafanya hivi wewe ni nani lakini? Mwanzoni ulisifiwa kwa kurudisha kiwango cha PP lakini ukasema wewe hujafanya lolote zaidi ya kumpa Nafasi tu PP mengine anafanya yeye mwenyewe! Uliulizwa juu ya Kiwango cha Iceman ukasema unafurahia kufanya kazi na Quality Players waliopo Manchester yaani Uwezo wao huwa huelewi uwaambie nini wafanye kipya maana kila kitu wanakifanya kwa Uwezo wa Juu sana hakuna Sifa hata moja unayostahili wewe bali wachezaji wenyewe You are such a Humble Guy, Ole dah! Sipati picha muda huu angekuwa yule Mkalimani hiyo mineno ya Shombo wapinzani wetu wangeikoga ?!

Ole

Juzi kati hapa kuna jamaa wakasema Tayari ushaishiwa mbinu baada ya Ile mbili mbili vs Burnley pale OT huku tukiisaka ile Sare kwa kumwaga Machozi, Jasho na Damu usiiiiiiku nini ulifanya Baada ya pale? Maana walikutabiria Mechi zako 10 tu, eti wachezaji wanacheza Jihadi wewe hujafanya lolote lile kwenye Team dah! Dunia hii lakini wewe upo Kimya na ukiendelea kusema unakabiliana na Mechi baada ya Mechi daima unaangalia mechi ya mbele hutazami mechi iliyoisha leo ama jana, Ole acha niliseme hili wewe ndio MMASAI pekee naeweza kumuamini kwa Sasa maana Miaka yote kulikuwa na Usemi huku kwetu Usimdhamini Mmasai atakuachia Shuka yaani nyinyi Wamasai hamdhaminiki wala hamuaminiki mwingine juzi tu hapa kawaachia watu FIMBO huko!

Sasa hebu nieleze juu ya Mechi ya Jana ndani ya Parc des Princess huku ukiwatumia Tahith Chong na Mason Greenwood kama Substitution zako muhimu unaibutua PSG pale pale Upenuni kwao na kuzima Kelele zote, Kuchana Mimakala yao, Wakazima Data na sasa Wametuacha wenyewe humu Mitandaoni tukitamba na wanatamani sana Waseme PSG wabovu ila sasa wataanzia wapi? Na kwasasa kale kamsemo Its Only Cardiff, It’s only Arse888, It’s Only Chelshit ? sikisikiii kabisa!

Ole Gunnar Solskjær wewe ni nani lakini? Na huwa unafanya nini pale Viunga vya Carrington? Ole uwa unawaambia nini Wale akina Angel Gomes? Hebu naomba Ratiba yako ya Siku nzima kuanzia ukiamka asubuhi, ukiingia Ofisini kwako, hadi ukitoka Ofisini kwako huwa unafanya nini haswa? David moyes ameshindwa ndani ya miezi 10, Aloysius Maria Paulus van Gaal Kocha Mjivuni alikuwa anademadema Mbili safi tatu chafu ndani ya miaka miwili, Hozee Dad Mlishi Mkalimani ndani ya miaka miwili na nusu na Mkataba mnono ameshindwa yaani Katika Mechi alizocheza msimu huu wote hajafika namna umeshinda Points nyingi na Mechi nyingi huku hakuna uliyopoteza yaani Mechi 17 Droo 2, Kupoteza 1 kushinda 14 huku katika hizo mechi zote 17 tukipata ushindi Mfululizo wa Mechi 9 za Away wewe ni nani Haswa lakini?

Ole Sosopi Sululu The Great White Maasai hebu niambie muda huu kama niamke ama niendelee Kulala? Mimi ni nani hata nigomee Amri yako ikiwa Unai Emery akiwa kwake mbeleya mke wake na watoto wake amekutii ?, Maurizio Sarri akiwa kwake na Sigara zake na wapambe wake amekutii ?, Tomas Tuchel huyu ndio alikuwa anahesabika kama Mkombozi wao tena pale PSG ndio kabisa baada ya akina Laurent Blanc, Unai Emery kufeli kuwapeleka kwenye Nchi yao ya Ahadi ya CL wakiwa wameweka Pesa hasa wale waarabu lakini pia Ametii amri yako mbele ya Washabiki wao na Familia yao ya Kifalme sasa mimi ni nani hasa hata nigome kukusikiliza NENO LAKO AMBALO NI AMRI KWAMBA NIAMKE AU NIENDELEE KULALA BAADA YA MKESHA WA JANA USIKU!

Ole wewe ushaamrisha huko watu wapigwe na wakapigwa mimi nije kutoka huku kwetu Magodigavilo tarafa ya Dihongole karibu kabisa na Kwedikwazu kwa akina Hombo Dikola Munyu eti nije kuanza kubishia AMRI zako ilihali sijui wewe ni NANI? Hapana siwezi kuwa mjinga kiasi hicho, NENO LAKO NITALITII HARAKA SAANA toa NENO MOJA TU NIENDELEE KULALA AMA NIAMKE?

Ole kuna Mtu kila muda ananiuliza kama Upewe MKATABA wa kudumu ama Lah! Nakosa jibu la kumpa maana ulipewa kama Caretaker hahahaha Ma Caretaker huwa wanadharaulika sana eti juu yako kuna mtu tayari mazungumzo yalikuwa yanaendelea kuchukua nafasi hiyo kama Permanent Manager baada ya miezi yako sita ila hadi hapa tulipofika yule mtu kaomba Asitishe mazungumzo maana walikuwa wanapiga mboyoyo Tukifungwa wa Sita, Tukishinda Wa Sita tukidroo wa Sita ila leo wamepotea na yule aliyekuwa anatajwa nae kazima Data ila Mimi siwezi jibu hili swali la wewe kupewa Mkataba wa kudumu hadi nifahamu kwanza wewe ni NANI HASWA?

Toka umefika EPL vitimu vyote vinatetemeka vinakuja kupigania Sare hata wale Kuku kishingo walipopata ile Suluhu walitoka na Vibe kama lote hivi yaani walishangilia kweli kweli kila tulipopata Majeruhi lakini kwasasa hawatamani hata kukuona, maana mwanzo walisema Eti nyuma yako yupo SAF ila kwa huu Moto wanasema hata SAF hakuweza kuufanya ndani ya siku 90 tu kwa sasa nao wameniomba nije nikuulize kwani wewe ni NANI HASWA LAKINI? Maana hawajui isije kuwa wanashindana na Mpango wa Mungu kuja kututoa kwenye Taabu na shida za Kelele zao kila KUKICHA!

Kuna Daktari mmoja jana wakati nasema TUNAVUKA KWENDA ROBO aliniambia IMANI yangu inakinzana na AKILI, nilimwambia IMANI sio kitu cha AKILI nilimwambia imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo na baina ya mambo yasiyoonekana hii ndio IMANI haina nasaba na AKILI lakini inahitaji kuwa UMEIVA KWENYE IMANI HASWA unafikiri Imani hii ililetwa na Lukaku? Ama Imani ile ililetwa na Tahith Chong? Ama Andrinho Pereira? Hapana Hii Imani haikuletwa na Uwepo wa De Gea golini Ole wewe ni nani Haswa? Hadi nitakapopata majibu ya maswali yangu nitarudi tena acha niendelee kusubiri majibu yako!

OLE GUNNAR SOLSKJÆR NAOMBA UNIPE MAJIBU NITULIZE AKILI YANGU WEWE NI NANI HASWA?

Imeaandaliwa na Dizo Moja

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.