Sambaza....

Nahodha wa timu ya Taifa ya Uganda “The Cranes” Dennis Onyango amesema Leo watajaribu kucheza kufa na kupona dhidi ya Cape Verde Ili kupata nafasi ya kushiriki kwenye michuano ya Mataifa Afrika kwa Mara ya pili mfululizo.

Onyango ameitaja mechi hiyo ambayo itapigwa katika uwanja wa Mandela uliopo Namboole Kama fainali ya ambayo ni lazima wacheze kwa moyo na ari kuweza kushinda na kufuzu michuano ya Afrika itakayofanyika mwakani nchini Cameroon.

“Ni lazima tucheze kwa kujituma na kwa moyo, tunajua thamani ya mechi hii, tunataka kurudi tena kwenye michuano ya Afrika, hii mechi ni kama fainali kwetu,” amesema Dennis Onyango ambaye ndiye kipa chaguo la Kwanza la timu ya Taifa.

“Cape Verde ni timu nzuri, lazima watacheza wakitafuta ushindi, lakini sisi tupo nyumbani na tuna hitaji kubwa zaidi, lengo letu ni kupata alama zitakazofanya tufuzu Hata kabla ya kwenda kucheza mechi ya mwisho dhidi ya Tanzania bila Kuwa na Pressure,” Ameongeza.

Uganda wanaongoza kundi L wakiwa na alama 10 katika michezo minne ambayo wamecheza hadi hivi sasa wakihitaji alama moja tu kujihakikishia nafasi ya kushiriki michuano ya AFCON 2019 nchini Cameroon itakayoshirikisha timu 24 kwa mara ya kwanza.

Sambaza....