Benno akiwa Yanga
Blog

Sababu kwanini BENO KAKOLANYA ni bora kuzidi AISHI MANULA

Sambaza....

Simba kwa sasa ina walinda milango wawili ambao wanaonekana ni bora sana, Beno Kakolanya ambaye alisajiliwa na Simba akitokea Yanga , pamoja na Aishi Manula ambaye amekuwa na kikosi kile cha Simba kwa muda sasa hivi , kiufundi tumejaribu kutazama nani bora kati yao na tumekuja na sababu kadhaa zinazombeba Beno Kakolanya kama golikipa bora mbele ya Aishi Manula.

REFLEXES

Moja ya matatizo makubwa kwa Aishi Manula ni Reflexes (uwezo wa kuzuia shots zinazokuja kwenye lango lake ). Mara nyingi hili eneo hayuko vizuri sana ukilinganisha na Beno Kakolanya. Beno Kakolanya kwenye Reflexes yuko vizuri , anaweza kuzuia shots zinazokuja kwa kichwa au miguu kuliko Aishi Manula.

UWEZO WA KUPIGA PASI

Moja ya tatizo ambalo Aishi Manula analo ni yeye kutokuwa na uwezo mkubwa wa kupiga pasi , na moja ya ubora ambao anao Beno Kakolanya ni kupiga pasi kuzidi Aishi Manula. Dunia ya sasa inahitaji magolikipa ambao wanauwezo wa kupiga pasi ndefu na fupi , Simba inatabia ya kuanzisha mashambulizi kutoka nyuma , unapokuwa unaanzisha mashambulizi kutoka nyuma unatakiwa uwe na kipa ambaye anauwezo wa kucheza pasi na hapa ndipo Beno Kakolanya anapomzidia Aishi Manula.

Manula

KUISHI KWENYE PRESHA YA MCHEZO

Moja ya kitu ambacho magolikipa wanatakiwa kuwa nacho ni uwezo wa kuivaa presha ya mchezo bila kufanya makosa mengi. Kuna wakati timu inakuwa haina mpira , timu pinzani inamiliki na kushambulia ndiyo wakati ambao kipa anatakiwa kuivaa presha na kuwa makini sana ili kuilinda timu. Beno Kakolanya anaweza kuivaa presha vizuri na kuendelea kuiweka timu ndani ya mchezo tofauti na Aishi Manula.

Beno Kakolanya

KUWAPANGA WACHEZAJI

Moja ya madhaifu ya Aishi Manula ni yeye kutokuwa na uwezo mkubwa wa kuipanga safu yake ya ulinzi. Hii ni tofauti na Beno Kakolanya amekuwa ni mtu ambaye ni kiongozi , kiongozi anayewapanga vizuri walinzi wake na kipindi wanapokosea huwakaripia kwa kuwaonya.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.