Blog

Safu ya ushambuliaji ilituangusha – Mgunda

Sambaza....

Jana kulikuwa na mechi ya kufuzu CHAN kwenye uwanja wa Taifa kati ya Taifa Stars na Sudan. Mchezo ambao Sudan walishinda goli 1-0. Baada ya mchezo huo kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” John Mgunda amesema kwamba safu ya ushambuliaji ndiyo iliyowaangusha.

“Kwanza kabisa nitumie nafasi hii kuwaomba radhi Watanzania wote , waandishi wa habari kwa matokeo ambayo tumeyapata”.

“Kiufundi tumetengeneza nafasi nyingi za magoli lakini hatujafanikiwa kufunga , hivo safu ya ushambuliaji imetuangusha kwa kiasi kikubwa”.

Alipoulizwa na Martin Kiyumbi mwandishi wa Kandanda.co.tz kama Taifa Stars inamkumbuka John Bocco , Kocha Mgunda alikataa.

“Timu inamhitaji mfungaji. Ndiyo maana tumetengeneza nafasi nyingi sana lakini hatujafunga magoli mengi ”

Martin Kiyumbi alimuuliza kwanini timu haiwezi kufunga. Chini ya Amunike timu ilifunga goli 2-0 dhidi ya Cape Verde, akaifunga Uganda 3-0 chini ya timu ambayo ilikuwa inacheza soka lisilo vutia , kwanini kipindi hiki timu inapocheza soka la kuvutia lakini haifungi magoli?

“Siwezi kuzungumzia falsafa ya mtu aliyepita lakini kwetu sisi mpaka sasa hivi washambuliaji wanatuangusha” alisema kocha huyo wa Coastal Union.

Taifa Stars itacheza mchezo wa marudiano dhidi ya Sudan nchini Sudan baada ya awali kuwepo taarifa ya mechi kuchezwa katika uwanja wa Nambole jijini Kampala nchini Uganda.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x