Sambaza....

Kuna swali ambalo huwa linaulizwa sana kila siku kuhusu hawa miamba wawili wa soka letu hapa nchini kwetu. Hawa ndiyo wamebeba jina la neno mpira kwenye soka letu kabisa. Hawa ndiyo wameigawanya Tanzania yetu katikati.

Kuna Tanzania nusu inaitwa Yanga hii ina rangi ya njano na kijani, na kuna Tanzania nyingine inaitwa Simba, hii ina rangi nyekundu na nyeupe. Kwa kifupi ni kwamba asilimia kubwa ya mashabiki wa mpira hapa Tanzania ni Simba na Yanga. Hizi timu zetu kwa kiasi kikubwa.

Huu ndiyo urithi wetu, tulirithi kwa mababu zetu. Hizi ni timu za mababu zetu ndiyo maana zina umri mkubwa sana na zina mashabiki wengi sana. Swali moja huwa linabaki moja tu ni ipi timu kubwa kati ya hizi ?, ukubwa wa timu huangaliwa kwa mambo mengi sana ambayo huifanya timu kuwa kubwa.

Ipi historia ya timu yako ?, timu yako ina historia gani ambayo hubeba hisia za wengi kibiashara?, hapa unaweza kutazama makombe. Makombe ambayo yamechukuliwa na vilabu husika na hapa unaweza ukathamanisha ukubwa wa vilabu vyote viwili.

Nia yangu sitaki kabisa kujikita huku, kuna sehemu naelekea. Sehemu ambayo imefanya mpaka nikae niandike hii makala.

Twende taratibu tutafika tu. Ukitoa historia ya kubeba makombe, kuna kitu kinaitwa “Fanbase” , idadi ya mashabiki ambao timu husika inamiliki. Kwa bahati mbaya timu zetu ni za wanachama. Kitu ambacho huwafanya mashabiki wengi kutochukua kadi za wanachama.

Ni wachache sana ambao wana kadi za wanachama, lakini wengi wao wanabaki kuwa mashabiki tu. Yani kwa kifupi mashabiki ni wengi kuliko wanachama.Na hakuna sensa maalumu iliyofanyika kuainisha Simba ina mashabiki wangapi na Yanga ina mashabiki wengi, hivo hii hoja hubaki juu juu tu.

Kuna kitu kingine kinaitwa utajiri wa klabu husika. Utajiri wa klabu husika hutazamwa kwa mali ambazo klabu husika humiliki. Hizi mali zinaweza kuwa fedha ambazo ziko kwenye bank. Gharama ya kikosi husika, Mali ambazo hazihamishiki , kama majengo, viwanja na miundombinu mingine.

Kitu kingine ambacho kinatufanya tuangalie ukubwa wa klabu ni nembo husika ya klabu kwa wakati huu. Klabu husika nembo yake (au chapa yake, kwa lugha ya kigeni Brand yake ina sura gani?).

Inatazamikaje kwa wakati huo, inavutikaje kwa wakati huo?, watu wanaishambuliaje?, wanaiongeleaje kwa wakati huo ?.

Sura ya chapa ya klabu kwa wakati husika ni kitu cha muhimu na cha msingi sana katika biashara, na hiki kitu ndicho husababisha wadhamini wengi kuvutika kwenda kuweka pesa.Kuna wakati chapa ya Taifa Stars ilikuwa inavutika sana hasa hasa kipindi cha Marcio Maximo. Ndicho kipindi ambacho watu wengi waliweka pesa zao pale.

Ndicho kipindi ambacho wachezaji waliishi maisha kama mtoto wa Mfalme. Hawakuwa na njaa kabisa, akili yao ilikuwa inafikiria kucheza mpira tu.

Kipindi hiki waliwahi kukipata Mbeya City wakati wanapanda ligi. Chapa yao ilikuwa bora na kubwa sana. Ilikuwa inavutia sana. Ilikuwa inazungumziwa sana, ndiyo maana ilifanikiwa kupata wadhamini wengi, nahisi ndiyo klabu ya kwanza kuwa na wadhamini wengi.

Hii ni kwa sababu ya chapa yao ilikuwa inazungumzwa vizuri sana, kitu ambacho kiliwafanya wengi wa wafanyabiashara kuwekeza pesa zao. Na hiki kitu ndicho kilichonifanya nikae na kuandika makala hii. Kwa sasa chapa ya Simba ni kubwa sana kuliko chapa ya Yanga.

Kwanini ?, sababu ni moja tu , Simba inazungumzwa, inatazamwa sana kuliko Yanga kwa kipindi hiki.

Jana Simba ilitolewa kwenye hatua ya nusu fainali ya Sportpesa Cup. Lakini matokeo haya yalizungumzwa sana kuliko matokeo ya Yanga ambayo ilitolewa katika hatua ya awali. Unajua kwanini?, kwa sababu Simba tangu awali wamete ngeneza picha ya wao kuonekana wakubwa tu. Picha ambayo inawafanya watu wawazungumze sana.

Picha ambayo inawafanya watu wengi watamani kuiona Simba ikifanya vizuri tu kila siku. Moja ya kitu kikubwa ambacho Simba wamekifanya kwenye nembo yao ni mapinduzi ya uongozi. Mapinduzi ya kuonekana Simba inamilikiwa na mtu kwa sasa. Hii inawafanya watu wengi waone Simba inaendeshwa kibiashara.

Kitu chochote kinachoendeshwa kibiashara siku zote hutazamia faida tu kwa kiasi kikubwa. Ndiyo maana watu wengi wanategemea na kusubiria matokeo makubwa kwa Simba. Ndiyo maana kila wakufungwa huandamwa zaidi kuliko wanavyoandamwa Yanga , na hii ni kwa sababu Yanga haijaamua kuishi Leo.

Ndiyo maana unakuta timu inatembeza bakuli kwa ajili ya kuomba pesa. Hii inashusha hadhi ya nembo/chapa ya klabu.Huwezi kuiona hii ni chapa ambayo inaweza kufanya vizuri kutokana na mazingira ambayo viongozi wao wameamua kuishi. kwenye maisha ambayo hawatakiwi kuishi, Simba wanajitahidi sana kuishi kwenye maisha ambayo ni sahihi kwao kuishi.

Ndiyo maana hawaogopi kusema kubwa kikosi chao ni cha bilionea moja. Wanajua kabisa wakitamka hivo wanaonesha thamani yao kubwa mbele ya watu wengi. Hata mfanyabiashara anapokuja kuwekeza pesa yake anajua anaenda kuwekeza kwenye timu yenye thamani kubwa sana.

Yanga bado wana nafasi kubwa sana ya kuifanya nembo yao Iwe kubwa. Wafanyeje?, jibu ni moja tu. hawamwihitaji Haji Manara ndani ya klabu.

Wanamwihitaji mwekezaji ndani ya klabu. Nitawaonesha mfano mmoja mzuri tu. Enzi za Yusuf Manji , thamani ya nembo ya Yanga ilikuwa inaonekana kubwa. Na hii ni siyo kwa sababu ya mdomo wa Jerry Muro, pesa za Yusuf Manji ndicho kilichokuwa kinaibeba Yanga. Na hiki ndicho kinachokosekana ndani ya Yanga na kinapatikana kwa Simba.

Simple tu, Yanga waamue kumpa mtu timu au timu iendeshwe kibiashara kwa sasa ili iweze kurudi tena kama kipindi kile , ili iweze kubwa na nembo kubwa na wao

Sambaza....