Mabingwa Afrika

Simba hata wakifungwa wanatakiwa kuwapigia makofi wachezaji.

Sambaza kwa marafiki....

Mashujaa !. Hawa ndiyo mashujaa wa vita. Vita ambayo ilionekana ngumu sana lakini mwisho wa siku hawa mashujaa waliifanya kazi kuwa nyepesi.

Unawezaje kuwabeza watu ambao waliwekwa kundi moja na wana Fainali wa michuano ya vilabu vya Afrika msimu Jana ?

As Vita alikuwa mwana fainali wa kombe la shirikisho barani Afrika msimu Jana. Al Ahly alikuwa mwana fainali wa ligi ya mabingwa barani Afrika msimu Jana.

Kundi lilikuwa gumu, lilikuwa limebeba watu ambao ni washindi wa vita. Watu ambao huwa wanajidhatiti sana kwenye kila vita wanayoingia.

Ndiyo maana huwa wanafanya vizuri sana kila wanapokuwa wanaingia kwenye michuano hii. Yani kwa kifupi Simba ilipangiwa kundi lenye timu ambazo michuano hii zimeumbiwa zenyewe.

Timu ambazo kufanya vizuri kwenye michuano hii imekuwa tabia ambayo ni ya kawaida sana kwao. Wameshaizoea.

Simba ndiyo kwanza haina tabia ya kufanya vizuri kwenye michuano hii. Kwa kifupi walikuwa wanaonekana ni timu ambayo Isingeweza kufanya vizuri mbele ya As Vita na Al Ahly.

Meddie Kagere na John Bocco wakiwa mbele ya Lango la Al-Ahly.

Hapa ndipo mwanzo wa kujivunia. Hapa ndipo mwanzo wa ushujaa wa wachezaji wa Simba unapoanzia.

Hapa ndipo uanaume wa Simba unapoanzia. Walifanikiwa kupita group la kiume. Kundi ambalo lilikuwa na wana fainali wawili wa michuano ya Afrika msimu Jana (ligi ya mabingwa barani Afrika na Kombe la shirikisho barani Afrika).

Na kizuri zaidi waliwafunga hawa wana fainali na kufanikiwa kufuzu kwenda hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

Huu ndiyo ushujaa ambao unatakiwa kutambulika. Sehemu ambayo Simba wamefikia ndiyo sehemu ambayo hata ukifa, unakufa huku unatabasamu.

Ndiyo sehemu ambayo huwezi kusikia maumivu ya kifo hata kama ukiwa unachinjwa kwa kisu shingoni mwako.

Mechi ya leo ni ngumu sana. Ni mechi ambayo inawakutanisha na timu ambayo ni ngumu. Timu ambayo ni kubwa barani Afrika.

Hata kama wakifungwa mechi wanatakiwa kabisa wasihuzunike. Wanatakiwa washangilie kwa nguvu zao zote.

Wanatakiwa kusimama huku wakiwapigia makofi wachezaji wao kwa kuwapongeza kufika Kwenye hatua ngumu kama hiyo.

Wamefika hatua ngumu baada ya kupita kundi ambalo ni ngumu. Simba hawatakiwi hata siku moja kuhuzunika kwa matokeo yoyote mabaya ambayo yanaweza kuwatokea.

Wanatakiwa kufa wakiwa wanatabasamu. Wamefanya kazi ambayo ni kubwa. Hawa ni mashujaa wakubwa sana. Mashujaa ambao wanatakiwa kupongezwa kwa nguvu zote.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.