Che Fonde Malone
Stori

Tigana: Huyu Che Malone ni Victor Costa Mtupu!

Sambaza....

Tayari Wekundu wa Msimba Simba wamecheza mechi tatu hapa nchini na baadhi ya wachezaji wapya waliosajiliwa msimu huu wameonekana.

Mchambuzi wa soka na mchezaji wa zamani wa Majimaji na Njombe Mji Tigana Lukinja yeye kwake jicho lake limenasa kwa mlinzo mpya wa klabu hiyo Che Fonde Malone.

 

Baada ya kuitazama fainali ya Ngao ya Jamii Tigana alisema “Kwa tuliyemuona na kucheza naye Victor Costa Nampoka na huyu Che Malone Fondo waweza kusema ni mapacha,” alisema na kiongeza;

“Sifa nyingi alizokuwa nazo Nampoka nyumba ndizo ambazo anazo Malone, utulivu wa hali ya juu ambao unatokana na uwezo mkubwa wa kuuchezea mpira.”

Che Malone akimthibiti Jesus Moloko.

“Pamoja na yote ni hali ya kujiamini  ambayo inaleta usahihi wa matendo ni kivutio kikubwa. Kuusoma mchezo nayo inamfanya kufanya vyema kwenye jukumu lake la ulinzi pale kikosini kwa Wanalunyasi.

Vitu ambavyo Nampoka “Nyumba” ndiyo alivyokuwa anavifanya wakati wake hapo hapo Msimbazi,” alimalizia Tigana

Sambaza....