Sambaza....

Wapwa, leo Wananchi wanacheza ugenini lakini ni nyumbani na Asas ya Djibouti katika mechi ya hatua ya awali ya Ligi ya mabingwa Afrika.

Nionavyo mimi kuna uwezekano mkubwa wa Hafiz Konkonii kama si kuanza basi kuingia akitokea benchi lakini nachotaka kusema hapa ni kwamba atapata muda mkubwa wa kuwepo uwanjani tofauti na game ya fainali kule Tanga.

 

Maana yangu kubwa hapa ni kuona uwezo wake kwa nafasi ya kutosha, kama nilivyowahi kusema anatajwa kuja kuvaa viatu vya mshambuliaji bora aliyeondoka ndani ya timu hiyo Fiston Mayele.

Sasa ikiwa atapata nafasi bila kujalisha uzito na ugumu wa mechi yeye binafsi anatakiwa aanze kuonesha vitu kama vya mtangulizi wake na ikiwezekana zaidi ya zaidi.

Hafiz Konkoni

Mfano Mayele kwenye mechi mbili dhidi ya Zaalan Fc alifunga magoli 6 itoshe kusema alikuwa na ujumbe mzito kuelekea mbele kwenye mashindano haya na mwisho wa siku akamaliza na goli saba katika kombe la Shirikisho Afrika.

Hivyo ni wakati wa Konkoni kutengeneza kujiamini na kutuaminisha wadau wa mpira kuna kitu amekihifadhi miguu.

Sambaza....