Blog

Wachezaji wa YANGA walikuwa wanakosa hata Elfu kumi – ZAHERA

Sambaza kwa marafiki....

 

Aliyewahi kuwa kocha mkuu wa klabu ya Yanga , Mwinyi Zahera amezidi kutoa maoni yake kuhusiana na klabu yake ya zamani . Jana alifanikiwa kuzungumza na mtandao huu wa kandanda.co.tz katika mahojiano maalumu.

Katika mahojiano ya jana aliulizwa atoe tofauti kati ya Yanga ya Luc Eymael na Yanga ambayo alikuwa anaifundisha na yeye akadai kuwa Yanga yake ilikuwa bora kuliko Yanga hii.

“Yanga yangu ilikuwa inacheza kwenye njaa na ilikuwa inashinda mechi , Yanga hii inapata kila kitu na inashinda kama Mimi nilivyokuwa nashinda wakati nikiwa na njaa”.

Kocha huyo alidai kuwa huwezi kuilinganisha timu inashinda vizuri mechi zake ikiwa na njaa na timu ambayo inashinda mechi zake ikiwa haina njaa.

Kikosi kilichoaanza dhidi ya Kagera Sugar

“Huwezi kulinganisha timu ambayo inacheza vizuri ikiwa kwenye njaa na timu ambayo inacheza vizuri ikiwa haina njaa. Mimi wachezaji walikuwa wanajituma wakiwa na njaa kitu ambacho ni kigumu”- aliongezea kocha huyo.

Kocha huyo amedai kuwa kuna wakati timu yake ilikuwa inalala kwenye hotel ambazo siyo za hadhi kubwa na walikuwa wanazuiliwa kuondoka kwa sababu ya kutakiwa kulipa madeni.

“Kuna wakati tulikuwa tunalala hotel za gharama za chini na tulikuwa tunashindwa kulipilia hivo tulikuwa tunakamatwa inabidi Mimi nilipe deni la timu” alidai kocha huyo

Kocha huyo aliongezea kuwa wakati wake timu yake ilikuwa ina safiri na gari umbali mrefu na timu ya sasa ina safiri kwa ndege kwenda kucheza mechi .

“Mimi wachezaji wangu walikuwa wakisafiri kwa gari tena umbali mrefu unafika mmechoka , wakati timu ya sasa wachezaji wanasafiri kwa ndege tu wanafika bila kuchoka”-alidai kocha huyo

Kocha huyo alimalizia kwa kujibu kuwa timu yake ilikuwa haina motisha kuilinganisha na timu ya sasa Lakini Tunu yake ilikuwa inashinda.

“Wachezaji wa sasa wnapata motisha wanamaliza mchezo wakiwa na laki tatu , wakati nafundisha wachezaji walikuwa wanakosa hata elfu kumi ya kurudi nayo nyumbani ”

“Inabidi ujitahidi kumjenga kisaikolojia mchezaji ili kesho acheze vizuri , mchezaji anayeenda nyumbani hana hata elfu kumi na inabidi wewe umpe tu hiyo elfu kumi” – alimalizia kocha huyo wa zamani wa Yanga

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.