Sambaza....

Wachezaji wa Yanga waliokua na Timu ya Taifa Tanzania  Kelvin Yondani, Hassan Kessy, Gadiel Michael na mshambuliaji Ibrahim Ajib wanatariwa kuondoka mchana huu kueleka mjini Morogoro kuungana na wenzao walioko kambini.

Ikumbukwe timu ya Yanga imeweka kambi ya muda jijini Morogoro kwajili ya maandalizi ya mchezo wa Azamsports Federation cup dhidi ya Singida utd. Mchezo huo utapigwa April Mosi 2018 katika dimba la Namfua Singida.

Yanga inatarajiwa kuwakosa baadhi ya wachezaji wake muhimu kutokana na sababu mbalimbali. Itamkosa kipa wake chipukizi Ramadhani Kabwili aliebaki ili kuitumikia Ngorongoro Heroes katika mchezo wa kufuzu AFCON U20 dhidi ya DR Congo. Pia itawakosa washambuliaji wake Yohana Nkomola na Amisi Tambwe walio majeruhi.

Sambaza....