
Klabu ya Yanga imesema kuwa, itakuwa imeshamilisha uwanja wake mmoja wa mazoezi hadi itakapofika Desemba mwaka huu.
- Kola na mfupa uliomshinda Mayele!
- George Mpole anaishi ndoto zetu!
- Alli Kamwe: Kumbe bila moto wanateseka!
- Kisa cha Kalilou Fadiga kuiba cheni.
- Azam kujimaliza yenyewe mbele ya Simba!
Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa klabu hiyo Dismas ten. Ten amesema kuwa mpango wa klabu ni kuwa na viwanja viwili, kimoja cha nyasi asili na kingine cha nyasi bandia ambavyo vitakidhi mahitaji ya klabu.
“Tuna eneo kubwa.. tunaweza kuweka viwanja viwili… kwa sasa uongozi unajitahidi kuhakikisha eneo hili linakamilika ili liwe tayari kuchezewa”
Yanga hutumia zaidi ya Milioni 36 kwa ajili ya kulipia viwanja vya mazoezi, hivyo uongozi wa klabu hiyo unaona kuharakisha kuwa na uwanja wake kutaokoa Mamilioni hayo.

“Uongozi upo makini kuhakikisha eneo hili linakuwa tayari kimatumizi ifikapo mwezi desemba mwaka huu..” alielezea Ten
Hadi sasa, inakadiliwa kuwa zoezi la kusawazisha eneo hilo limefikia 80% kukamilika huku klabu ikiwa na mipango mikubwa zaidi hasa kulizunguushia ukuta au majukwaa baada ya eneo hilo kukamilika kwa 100%.