Blog

Yaya Toure kufanya majaribio kwenye timu ya daraja la pili.

Sambaza....

Kiungo wa zamani wa Barcelona na Manchester City Yaya Toure yupo nchini China kwenye klabu ya Qingdao Huanghai akifanya majaribio kwa ajili ya kujiunga na klabu hiyo ya daraja la pili.

Klabu hiyo imetoa taarifa ya majaribio hayo kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 36 leo Ijumaa ambapo imesema kwamba jopo la makocha wataangalia kiwango chake ikiwemo hali yake ya kifiziki kabla ya kuamua kumsajili moja kwa moja.

“Yupo hapa kwa ajili ya majaribio, jopo la makocha wa klabu watamuangalia fiziki yake na uwezo wake kama anaweza kuitumikia klabu yetu,” Taarifa ya klabu hiyo imesema.

Mwishoni mwa mwezi uliopita wakala wake Dimitry Seluk alitoa taarifa kuwa Yaya Toure ambaye hakuwa na timu toka Disemba mwaka jana baada ya kukaa miezi mitatu pekee na Olympiakos ya Ugiriki kwamba amestaafu soka jambo ambalo Yaya Toure mwenyewe alilipinga na kusema kuwa bado ana uwezo wa kucheza soka kwa miaka kadhaa ijayo.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.