Blog

Zahera siyo kocha wa Gwambina FC

Sambaza....

Kuliripotiwa habari za urejeo wa aliyewahi kuwa kocha mkuu wa klabu ya Yanga , Mwinyi Zahera katika ligi yetu. Mwinyi Zahera aliwahi kuhudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja kwenye ligi kuu akiwa kocha mkuu wa Yanga.

Picha zilienea zikimuonesha Mwinyi Zahera akiwa na viongozi wa Gwambina FC , timu ambayo imepanda ligi kuu msimu na makao makuu ya timu hiyo ni Misungwi mkoani Mwanza.

Wakizungumza na mtandao huu wa kandanda.co.tz viongozi wa Gwambina FC wamedai kuwa  Mwinyi Zahera atakuwa mkurugenzi wa ufundi wa Gwambina FC.

Mwinyi Zahera atasimama kwenye ukurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo. Benchi kuu la ufundi litaongozwa na Frugence Novatus ambaye ndiye kocha mkuu na aliyeipandisha timu , kocha msaidizi atakuwa Hassan Bilali “Bilo”


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.