Martin Kiyumbi

Mchambuzi
Mchambuzi wa mpira wa miguu, mwenye Shahada ya Ualimu. Martin amejiunga na timu ya kandanda toka mwaka 2017, moja kati ya wachambuzi wakongwe katika familia yetu.
Ligi Kuu

Aliye karibu na Kichuya amng’ate sikio ‘fastaaa’.

Misimu miwili imeshakamilika akiwa katika ardhi yenye udongo mwekundu, udongo ambao upo kwenye mbuga ya msimbazi, mbuga pekee yenye mnyama mmoja yani Simba. Mbuga hii ina malisho ambayo yana unafuu kuzidi mbuga zingine za mikoani, ndiyo maana wengi wa wachezaji hutamani sana kuishi kariakoo wakiamini ni sehemu yenye unafuu mkubwa...
Mabingwa Ulaya

Ni Real Madrid tena? Au Liverpool?

Ulevi wa timu hizi kwenye Ligi ya Mabingwa utatia ugumu wa mchezo? Hapana shaka kwa sababu zinakutana timu ambazo ulevi wao mkubwa ni michuano hii ya Ulaya, damu huchemka na wehu uingia akilini mwa kila mchezaji wa timu hizi linapokuja suala la Ligi ya mabingwa barani ulaya. Real Madrid wanatafuta...
Ligi Kuu

Nilichojifunza kwenye kipigo cha Simba dhidi ya Kagera Sugar.

Leo hii Simba ilikuwa inacheza mechi ambayo wangekabidhiwa kombe lao , furaha kubwa kwao ilikuwa ni kukabidhiwa kombe wakiwa hawajafungwa hata mechi moja kwenye ligi kuu lakini Juma Kaseja akaharibu matamanio yao. Kipi nimejifunza kwenye mechi hii? 1: Hapana shaka Watanzania tunapenda matukio ya muda mfupi na siyo matukio ya...
Blog

Lwandamina alijijenga yeye na kuiua Yanga.

George Lwandamina ni moja ya jina kubwa barani Afrika kwa sasa, huwezi kukwepa ukweli kuwa George Lwandamina aliwahi kufanya vizuri kwenye michuano ya vilabu barani Afrika akiwa na Zesco United ya Zambia. Inawezekana kabisa hii ilikuwa moja ya sababu ambayo iliwashawishi Yanga wamchukue George Lwandamina ili wafikie mafanikio makubwa kwenye...
Shirikisho Afrika

Maeneo ya kuwapa ushindi Yanga

1: Golikipa. Moja ya eneo ambalo ni muhimu kwenye timu ni eneo la golikipa, siku zote golikipa ndiye mshambuliaji wa kwanza na ndiye mtu ambaye anaifanya timu iwe hai muda mwingi mwa mchezo. Lakini hii imekuwa tofauti sana kwa Youthe Rostand. Amekuwa golikipa ambaye ana makosa mengi akiwa langoni. Mfano...
Ligi Kuu

Mpaka sasa Manara hajui kushoto na kulia.

Muungurumo ni mkubwa mno tena wenye nguvu kubwa sana kutoka katika mbuga ya msimbazi, mbuga ambayo haikuwa na malisho kwa muda wa misimu minne (4). Misimu minne (4) imekuwa misimu yenye mateso na njaa kali sana kwa Simba anayepatikana katika mbuga ya msimbazi. Kila kitu kilikuwa kigumu kwake hata afya...
Ligi Kuu

Jasho la KDB limeivaa jezi ya Kichuya.

Hapana shaka ndiye mchezaji bora wa Simba na wa ligi kuu msimu huu, hili ndilo neno pekee ambalo ninaweza kuanza nalo ninapoandika makala hii. Shiza Ramadhani Kichuya alisifiwa sana wakati anakuja msimbazi na mimi sikutaka kumsifia nilimpa tafadhari moja tu kwenye andiko langu "Kichuya karibu kwenye kioo cha kinyozi". Kioo...
Ligi Kuu

Simba yachukua ubingwa ikiwa chumbani.

Baada ya kukaa misimu minne bila kuchukua ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara, hatimaye klabu ya Simba imefanikiwa rasmi kuwa bingwa wa Ligi kuu Tanzania bara msimu wa mwaka 2017/2018. Hii imetokana baada ya timu ya Prisons kuifunga Yanga magoli 2-0 . Kwa matokeo hayo Simba ina alama ambazo haziwezi...
Ligi Kuu

Teke la Azam kwa John Bocco, limeongeza mwendo wa chura.

Kuna mengi ya kujifunza kwenye safari ya Arsene Wenger akiwa Arsenal. Watu wengi hatukumjua kitu ambacho kilifanya tusimwamini kabisa. David Dein pekee alikuwa na imani dhidi ya Arsene Wenger, ungeanzaje kumwaminisha shabiki kuwa kocha anayetoka katika ligi ƴya Japan angekuja kuipa mafanikio Arsenal? Hakuna mafanikio yaliyoonekana mbele ya mashabiki wa...
1 66 67 68 69 70 79
Page 68 of 79