Mabingwa Ulaya

Ni Real Madrid tena? Au Liverpool?

Sambaza....

Ulevi wa timu hizi kwenye Ligi ya Mabingwa utatia ugumu wa mchezo?

Hapana shaka kwa sababu zinakutana timu ambazo ulevi wao mkubwa ni michuano hii ya Ulaya, damu huchemka na wehu uingia akilini mwa kila mchezaji wa timu hizi linapokuja suala la Ligi ya mabingwa barani ulaya. Real Madrid wanatafuta kombe lao la kumi na mbili (12) wakati Liverpool wakitafuta kombe lao la sita (6).

Eneo la ulinzi la timu zote.

Mwanzoni mwa msimu Liverpool ilikuwa na mapungufu mengi sana katika eneo la kuzuia. Lakini usajili wa Van Djik umekuwa na msaada mkubwa kwa sababu hakuna makosa binafsi katika eneo hili la nyuma na amekuwa kiongozi mzuri katika eneo hili la nyuma la Liverpool, mpaka sasa hivi Liverpool wamepata clean sheets (6) katika michezo kumi na mbili (12) msimu huu wakati Real Madrid wamepata Clean sheets 3 katika michezo 12 ya ligi ya mabingwa msimu huu na wakifungwa magoli 12.

Kipi kinasababisha ionekane ukuta wa Real Madrid kuwa mbovu?

Sehemu kubwa ambayo Real Madrid huruhusu magoli ni sehemu ya beki wa kushoto anapocheza Marcelo. Muda mwingi Marcelo huonekana katika eneo la mpinzani kuliko katika eneo la kujilinda ndiyo maana magoli mengi hupitia kwake.

Eneo la kiungo kwa timu zote likoje?

Eneo hili limebeba watu ambao hawaangaliwi sana lakini ndiyo watu ambao wamebeba mipango ya timu zote mbili.

Casemiro, amekuwa akilinda mabeki wake vizuri na hii imekuwa ikiwapa nafasi Toni Kroos na Luka Modric kusogea mpaka eneo la mbele kutengeneza nafasi.

Wakati Liverpool wana James Milner ambaye amehusika katika utoaji wa pasi nyingi za mwisho wa magoli msimu huu wa Ligi ya mabingwa akiwa na pasi nane (8) za mwisho.

Kushuka kwa BBC na Kupanda kwa Utatu mtakatifu wa Liverpool.

Mpaka sasa Firmino, Salah na Mane wamefunga magoli 29, wakati Mara ya mwisho kwa Benzema, Bale na Ronaldo (BBC) kufunga magoli mengi kwenye michuano hii ya Ulaya ilikuwa msimu wa mwaka 2013/2014 walipofunga magoli 28 kwa pamoja.

Kipi kimesababisha kushuka kwa BBC?

Majeraha ya Mara kwa Mara ya Gareth Bale yamerudisha nyuma maendeleo ya BBC pamoja na kushuka kwa kiwango cha Karim Benzema ambaye msimu huu amekuwa na msimu wa kupanda na kushuka.

Wakati BBC wakishuka, Muunganiko wa Firmino, Salah na Mane umekuja katika sehemu kubwa na imekuwa muunganiko ambayo unatisha zaidi msimu huu.

Kuna nafasi ya Mohammed Salah kuwang’ara?

Nafasi ni kubwa sana. Kwanini? Moja ya sababu ambayo nimeielezea inayosababisha RealMadrid kufungwa ni eneo lao la kushoto kuwa dhaifu kwenye suala la kujilinda.

Hivo hii itampa nafasi Mohammed Salah kuwa huru eneo hili kwa sababu Marcelo atakuwa anatumia muda mwingi mwa mchezo katika eneo la mpinzani kuliko eneo lake.

Ronaldo ana nafasi kubwa ya yeye kung’ara pia?

Hapana shaka, kwa sababu moja ya silaha ambazo humfanya ang’are zitakuwepo. Silaha zenyewe ni Marcelo na Carvajal ambao wamekuwa ni chachu kubwa ya mashambulizi kwa Real Madrid.

Mchezo utaisha vipi?

Mchezo huu una nafasi kubwa ya kumalizika kwa magoli mengi ambayo timu zote zitafungana na hii ni kwa sababu ya mechi tatu zilizopita za timu hizi, mechi hizi zimeonesha timu hizi zinaweza kufungwa magoli kipindi ambapo presha kubwa inapokuwa kwao. Timu zote zinawachezaji ambao wanauwezo wa kutia presha ndiyo maana kuna nafasi kubwa ya mchezo huu kumalizika kwa magoli mengi.

TABIRI USHINDE


Nenda chini ya ukurasa huu uandike utabiri wako (sehemu ya ‘comment, kwa facebook) wa mechi hii kwa Kutaja Idadi ya Magoli, Mchangiaji wa kwanza kutabiri sahihi atajishindia jezi ya timu iliyoshinda kutoka duka la vifaa vya michezo la ZIZZOU FASHION na fulana moja ya GALACHA.
(Hakikisha comment zako kwa facebook ni ‘public’ au ‘open’ ili kila mtu aweze kuziona)

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x