Martin Kiyumbi

Mchambuzi
Mchambuzi wa mpira wa miguu, mwenye Shahada ya Ualimu. Martin amejiunga na timu ya kandanda toka mwaka 2017, moja kati ya wachambuzi wakongwe katika familia yetu.
Ligi Kuu

Kuna wakati Manara anajing’ata ulimi wake.

Instagram ndiyo sehemu ambayo watu wengi maarufu hapa nchini kwetu hutumia kuonesha maisha yao binafsi na maisha ya biashara zao. Kwenye dunia hii ya sasa kila kitu ni biashara, na ili ufanikiwe kwenye kila kitu unachokifanya lazima ukifanye kwenye jicho la biashara. Ndiyo maana Diamond Platnumz aliondokana na dhana ya...
Blog

Tutumie hata kitabu cha Samatta kwa kina Ajib

Dibaji yake inavutia na haitofautiani sana na Dibaji za wachezaji wengi wa Tanzania. Hakuzaliwa katika mazingira yenye utajiri mkubwa, hata hakufanikiwa kuwa kwenye vituo vya kulelea na kukuza vipaji. Kwa kifupi ametokea kwenye mazingira halisi ya kitanzania. Mazingira ambayo vijana wengi hupitia. Mazingira ambayo yalimpa nafasi ya kucheza chandimu. Ndiyo...
EPL

Tatizo linaanzia kwenye Kivuli cha Ferguson

Alama yake aliitumia kuiweka kwa miaka 27, umri wa mtu mzima. Akili, nguvu na muda wake mwingi aliuwekeza katika maisha ya Manchester United. Ndiyo maana alifanikiwa kuwa kocha mwenye mafanikio makubwa sana katika klabu ya Manchester United Alihakikisha kila sekunde inayopita katika maisha yake ilikuwa ni muhimu kuwapa furaha mashabiiki...
Blog

Mwambieni baba yake Kelvin John, nimemwandalia kahawa.

Vingi vizuri vimepita lakini havikufika sehemu ambayo vilitakiwa kufika na ndiyo maana wengi husema utajiri mkubwa upo makaburini. Watu wanakufa na mawazo yao makubwa ambayo walishindwa kuyafikia wakiwa duniani kwa sababu ya mazingira magumu ambayo yalisababisha kutofikia sehemu waliyoota. Hii ni dhambi kubwa sana, dhambi ambayo hukumu yake ni majuto...
EPL

Tatizo gari alilopanda Pogba, Dereva ni Raiola!

Pesa zilianza kumzoea mapema sana. Hakuweza kukaa bila na pesa yoyote mfukoni mwake tangu akiwa mtoto. Kwake yeye pesa kilikuwa kitu muhimu sana kuliko mwanamke. Vijana wengi wanapofikia umri wa kubalehe huwa machizi wa kutamani kuwa na wanawake wengi, lakini kwake ilikuwa tofauti kabisa. Alikuwa binadamu mwenye asili nyingine na...
Ligi Kuu

Tofauti kati ya Simba ya Lenchantre na ya Patrick.

Nchi nzima ilikuwa Mwanza. Masikio yetu yaliazimwa miamba, macho na akili zetu zikasafiri kwa njia ya maji mpaka Mwanza. Ngao ya jamii lilikuwa tukio ambalo lilifanyika Mwanza na kwa kiasi kikubwa kulikuwa na mafanikio makubwa sana hasa hasa  kwenye hamasa ya mashabiki kuingia  kwa wingi uwanjani. Simba ndiye mabingwa wa...
Ligi Kuu

Naisubiri kesho ndipo nimsifu Karia.

Wallance Karia ndilo jina ambalo wazazi wake waliamua kumpatia, sijui kichwani mwa wazazi wao walikuwa wana waza nini kuhusu maisha ya baadaye ya mtoto wake. Kama ilivyo kwa wazazi bora bila shaka picha ya maisha mazuri ya mtoto wao kwa siku za baadaye ilikuwepo kichwani mwao. Hiyo ndiyo fahari ya...
Ligi Kuu

Cannavaro, Udongo tunaopenda kuupuzia

Zanzibar ndipo kitovu chake kilipozikwa, kitovu ambacho kilikuwa na siri kubwa, siri ambayo ilikuwa inaonesha kuwa kuna mwanasoka imara kazaliwa katika ardhi hiyo. Mwanasoka ambaye mpaka anamaliza maisha yake ya soka kafanya dhambi moja tu nayo ni dhambiya kutocheza soka la kulipwa. Alikuwa na vigezo vingi ambavyo vingemwezesha kuwa mchezaji...
Tahariri

Tunawekeza ubora wa paa la Taifa Stars na kusahau msingi.

Fikiria neno "hatua" ni neno dogo lakini ndilo limebeba tafasri halisi ya neno maendeleo. Maendeleo ni wingi wa hatua zinazopigwa kimahesabu, haijalishi ukubwa wa hatua ambazo mtu anapiga cha muhimu ziwe hatua za kwenda mbele. Katika safari ya maisha ni ngumu kuanzia hatua ya tano bila kuanza hatua ya kwanza....
1 64 65 66 67 68 79
Page 66 of 79