Timu ambayo ilikuwa inasubiriwa kushuka daraja kuungana na African Lyon imepatikana rasmi. Kagera Sugar ya Kagera imeshuka rasmi baada ya kutoka sare moja kwa moja na Mbao.
Ratiba ambayo sio rafiki kwa upande wa Lipuli FC imebidi wafanye hivi ili kuipa umuhimu fainali yao itakayowapa tiketi ya kuwakilisha Tanzania katika michuano ya Afrika.
Taarifa ambazo tovuti yetu imezipata ni kwamba kilichomkwamisha Ajibu kwenda TP Mazembe ni biashara ambayo imefanywa kati ya Ajibu na Simba kabla ya ofa ya TP Mazembe kutua mezani kwa klabu ya Yanga.
Bado anajiona anataka kuendelea kukaa nyumbani, na amekataa kwenda sehemu ambayo inaweza kumwezesha yeye kushinda taji la ligi ya mabingwa barani Afrika.