Blog

Kagera Sugara yashuka rasmi daraja

Sambaza....

Timu ambayo ilikuwa inasubiriwa kushuka daraja kuungana na African Lyon imepatikana rasmi. Kagera Sugar ya Kagera imeshuka rasmi baada ya kutoka sare moja kwa moja na Mbao.

Stand United ya Shinyanga ambaye alikuwa mpinzani wa Kagera Sugar licha ya kufungwa na JKT Tanzania kwa goli 2-0 na JKT Tanzania amebaki ligi kuu.

Timu hizi zimelingana alama kwa kuwa na alama 44 kila mmoja. Kwa mujibu wa kanuni za ligi kuu ya Tanzania bara zinaelekeza kutazama michezo ambayo timu husika zilikutana.

Kagera Sugar na Stand United katika mchezo wa kwanza zilitoka sare ya moja kwa moja, na mechi ya pili Stand United walishinda kwa goli 3-1. Hivo matokeo haya yameifanya Stand United kubaki.

Timu mbili ambazo zitacheza playoff (Michezo ya mitoano ) ni Kagera Sugar aliyeshika nafasi ya 18 na Mwadui FC aliyeshika nafasi ya 17.

Mwadui na Stand United watacheza na Pamba FC ya Mwanza na Geita Sports ya Geita. Mshindi wa playoff atapanda ligi kuu Tanzania bara msimu ujao tena


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.