Sambaza....

Sina tatizo na Tff wala kamati zake na hata muda uliotumika kupitia vielelezo pia naona ulikuwa sahihi kabisa kutokana na uhalisia wa jambo lenyewe

Ndio ilikuwa sahihi kwa maana Obrey Chirwa aliitwa na Tff, lakini alikuwa kwao Zambia akifanya shughuri zake za kilimo na hata aliporudi nchini aliunganisha Zanzibar kwenye kombe la mapinduzi hapa bado kamati ya nidhamu ilikuwa sahihi, isingeweza kutoa adhabu bila kimsikiliza Chirwa……hapa ndugu msomaji unapaswa uelewe vizuri, kuwa kamati baada ya kumsikiliza Obrey Chirwa  ndipo imetoa adhabu hiyo kwa mujibu wa kanuni za ligi kuu kanuni ya 37(b) na kanuni za nidhamu za TFF kifungu cha 48 (1d) na 48 (2)

Ila tatizo langu lipo kwa huyu Obrey Chirwa, mara kwa mara amekuwa akikumbwa na makosa ya namna hii itakumbukwa mchezaji huyu alilipotiwa kumpiga mwandishi wa habari na kuharibu vitendea kazi vya mwanahabari huyo, kabla ya kufanya tena kosa kama hilo kwa kumpiga mchezaji wa Tanzania Prisons kwa makusudi hali inayopelekea kufungiwa michezo mitatu na faini ya shilingi laki tano.

Ukiyatazama kimsingi haya ni makosa ya kinidhamu na hapa ndipo kwenye tatizo la mchezaji huyu, maoni yangu kwa watu wa karibu na mchezaji wanapaswa kumuweka chini na kuzungumza naye ili aondokane na tatizo hili kuliko kumuaminisha vitu tofauti

Ndio wanapaswa kumuweka chini kwa maana nionavyo mimi Chirwa anahitaji kupewa darasa, litakalomfanya kutambua nini maana ya mchezaji kuwa na nidhamu na kazi gani iliyomleta nchini, inawezekana akawa amesahau lakini huo utakuwa ukumbusho kwake mwisho akawa ni mchezaji mwenye nidhamu kubwa

Chirwa anapaswa kuwa muungwana kwa maana mchezo wa mpira wa miguu sio vita (ni mchezo wa kiungwana) na anapaswa kutambua kuwa kukosekana kwake kwenye kikosi kunaighalimu timu (Yanga sc) ambayo kwa sasa inapambana kutetea taji lake la ligi kuu

Binafsi naamni Chirwa ni mchezaji mzuri sana mwenye uwezo wa kuisadia timu yake……lakini suala la nidhamu anapaswa kulizingatia sana ili wachezaji vijana waweze kijifunza kwake

Karamu yangu inaishia hapa huku ikiacha ujumbe wa Fair play

Sambaza....