Uhamisho

Nyota watakaompisha Ten Hag United wakiongozwa na Pogba

Sambaza....

Huku mipango ya kuijenga upya United ikiwa tayari imethibitishwa na bosi wa muda Ralf Rangnick, wachezaji watano wanakaribia kuondoka katika klabu hiyo kwani mikataba yao itamalizika mwezi Juni, huku kukiwa hakuna  dalili za kuongezwa mikataba.

Nyota hao ni Paul Pogba, Jesse Lingard, Edinson Cavani, Juan Mata, na Lee Grant . Kiungo wa kati wa Serbia Nemanja Matic, ambaye pia mkataba wake ulikuwa unamalizika mwishoni mwa msimu huu tayari ametangaza kuachana na timu hiyo mpango wake wa mwisho wa msimu huu, na hivyo kuhitimisha kukaa kwake kwa miaka mitano Carrington.

Paul Pogba

Pengine moja ya majina ya kushangaza zaidi ya wababe hao wa Uingereza wanasemekana kuwa tayari kuondoka katika klabu hiyo ni mhitimu wa akademi Marcus Rashford.

Mwingereza huyo amekuwa na msimu mbaya katika jezi nyekundu msimu huu akiwa amechangia mabao matano pekee na asisti mbili katika mechi 30 za mashindano yote, na kulingana na The Sun, Mashetani Wekundu wako tayari kumuachia nyota huyo mwenye  miaka 24 ambaye mkataba wake unaisha Juni 2023.

Marcus Rashford

Pia  mmoja wa wachezaji waliokaa muda mrefu zaidi kwenye mabingwa hao mara 20 wa Uingereza, Phil Jones, nae amepewa nafasi ya kujiunga na timu mpya msimu ujao, ingawa mkataba wake unamalizika mwaka ujao.

Majina mengine ambayo yameripotiwa kuwekwa kwenye kikosi cha kuondoka United   ni pamoja na mabeki wa pembeni Alex Telles na Aaron Wan-Bissaka .


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.