Zana atakumbukwa zaidi na jamii ya wana Simba kutokana na muonekano wake wa kipekee, ukaribu na mashabiki , vituko na aina ya uchezaji wake wa kupiga krosi yaani kumwaga maji na yakamwagika.
Amepiga “successful tackle” moja, alitumika kama winga wa kushoto. Pale alipopata nafasi ya kushambulia, alifanya hivyo na alileta madhara, ndio maana ya goli lake. Anastahili kupata alama alizo zipata
Tabiri matokeo kwa kuandika katika sehemu ya maoni ndani ya tovuti yetu tu ya mechi hiii. Mtu wa kwanza kuwa sahihi kabla ya mchezo kuanza atajipatia tiketi ya VIP B mechi ya Simba SC vs AS V.Club na Jezi ya Klabu ya Simba.
Katika msimamo wa kundi D Simba inashika nafasi ya tatu baada ya kucheza michezo miwili, wakishinda mchezo mmoja dhidi ya Jeunesse Sportive de la Saoura kwa mabao 3-0 jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda kupokea kichapo kikali cha mabao 5-0 kutoka kwa AS Vita ya nchini DR Congo