EPL

Maeneo matatu anayotakiwa kurekebisha ARTETA pale ARSENAL

Sambaza....

Tayari Arsenal iko na Mikel Arteta kama kocha mkuu wa Arsenal , kocha ambaye aliwahi kuhudumu pale kama mchezaji kwa muda wa miaka sita (6) anarudi tena Arsenal wakati ambao Arsenal inafanya vibaya , kipi afanye kwa haraka ainasue ?

KUCHEZA HIGH DEFENSIVE LINE.

Moja ya kitu ambacho Arsenal kwa sasa inasumbuka ni makosa mengi katika idara ya ulinzi , Sokraits na David Luiz wamekuwa wakifanya makosa mengi binafsi. Kwangu Mimi makosa haya yanayofanyika kwenye idara ya ulinzi yanatokana na umbo la timu na siyo kiwango cha wachezaji.

Kiwango cha wachezaji ni kikubwa , lakini umbo la timu linaloweza kuendana na kiwango chao ndiyo tatizo, kipi Mikel Arteta afanye ? Mikel Arteta anatakiwa kwa haraka aiwezeshe timu iweze kufanya Pressing na Kushambulia.

Mane langoni mwa Arsenal

Moja ya njia nzuri ya kufanikisha hiki ni kucheza High Defensive Line , mabeki wa katikati wanajipanga kuanzia katika ya uwanja, mabeki hawa wa Kati wao ndiyo wanakuwa watu wa kwanza kufanya Pressing , pia watawafanya wapinzani wacheze kwenye nusu yao kwa kuwalazimisha.

KUKABIA JUU (HIGH PRESSING).

Mwanzoni mwa Unai Emery alifanikiwa kwenye hili ila baadaye likawa linapotea , najua Arteta ametoka kwenye mikono ya Pep Guardiola, mikono ambayo mara nyingi husisitiza timu yake isikae bila na mpira ndani ya sekunde 30, ikipoteza mpira ihakikishe inaupata ndani ya sekunde 30, hiki kitu kinatakiwa kufanyika kwa Arteta , Arteta anatakiwa afikirie namna ambavyo atakuwa na uwezo wa kukabia juu ili kutowapa uhuru mabeki wa timu pinzani kuanzisha mashambulizi na timu pinzani kuwa na mpira.

KUTUMIA MABEKI WA PEMBENI KAMA VIUNGO WA KATI

Aina ya mabeki wa pembeni wa Arsenal mara nyingi kiasili hupanda sana , hiki kitu kilipotea ingawa mwanzoni mwa ujio wa Unai magoli mengi yalikuwa yanapatikana pembeni mwa uwanja. Kitu pekee ambacho Arteta anatakiwa kukifanya kwa haraka ni yeye kuruhusu viungo wake wa Kati kusogea mbele zaidi , nafasi zao zinazobaki katikati mwa uwanja zizibwe na mabeki wa pembeni , wakati huo pembeni mwa uwanja kuwepo na wingers wanaokaa pembeni mwa uwanja tu ili kuwavuta mabeki wa pembeni wa timu pinzani kuwafuata, wanapowafuata uwazi nyuma uwazi ambao utatumiwa na viungo wa Kati wa Arsenal wanaopanda mbele huku nyuma nafasi zao zikiwa zimezibwa na mabeki wa pembeni. Hii itaongeza idadi ya watu mbele na kuisaidia Arsenal kupata mafanikio kwa kipindi hiki kifupi.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.