Mason Greenwood
EPL

Wazungu Wanavyopata Tabu na Sakata la Greenwood

Sambaza....

Manchester  United ilipanga kurekodi video ya Mason Greenwood inayoelezea uamuzi wa kumrejesha mshambuliaji huyo chipukizi katika kikosi chake tena.

Afisa Mtendaji mkuu wa Manchester United Richard Arnold alipanga kuachia video inayoeleza hasa kwa nini Mason Greenwood alirudishwa kikosini, inasemekana.

 

Klabu hiyo iliripotiwa kulenga kutoa ujumbe huo wa video kwa wafanyikazi na mashabiki mnamo Agosti 4 n kutangaza kurejea kwa mshambuliaji huyo Muingereza.

Richard Arnold, Mkurugenzi Mtendaji, angeelezea mpango wa namna gani Greenwood angejumuishwa tena kwenye timu hiyo kama zamani baada ya kumaliza kesi yake.

Mason Greenwood

Upande wa Pili!

Kocha mkuu wa Manchester Unitd ameonyesha ni wazi anamuhitaji mshambuliaji huyo kikosini kutokana na uhitaji wa washambuliaji zaidi. Tayari kikosini ana Anthyo Martial (ambae amekua akikumbwa na majeruhi mara kwa mara) na Marcus Rashford pamoja na nyota mpya Rasmus Hojlund kutoka Atalanta.

Asubuhi ya Jana Gazeti la “The Mirror” kupitia kwa Mwandishi wao Henry Moore liliripoti kuwa bado muafaka haujapatikana.

Marcus Rashford.

Chaguo la Mason Bado halijafahamika iwapo Greenwood atarejea kwenye mazoezi ya kikosi cha kwanza au atatolewa kwa mkopo wa msimu mzima.

Vyanzo vya habari vilisema Greenwood anapinga kuhamia nje ya nchi na Man United wanasita kumtoa kwa mkopo kwa mpinzani wake wa Ligi Kuu.

Sambaza....