Blog

Afisa Masoko hili linawahusu kwenye VPL.

Sambaza....

Ligi Kuu Bara inayojulikana kama Vodacom Premier League inaendelea kushika kasi ikiwa inaelekea ukingoni. Ligi itaenda itakwisha na msimu mwingine utaanza tena na macho na masikio ya wapenda soka wataendelea kuifwatilia.

Wakati mwingine inashangaza kidogo kwa ligi yetu hii pendwa inayotoa burudani na ushindani wa hali ya juu huku ikionyeshwa live kupitia Azamtv kuona timu zinacheza zikiwa hazina nembo au tangazo lolotee kifuani mwao, yani nikimaaminsha baadhi ya timu  hazina wadhamini.

Hapo ndipo nawakumbuka maafisa masoko “Marketing  Managers” wa kampuni mbalimbali za Tanzania na baadhi wa nje ya Tanzania.

Hivi ni kweli wameshindwa kuzishawishi kampuni zao kuingia katika vilabu na kuweka udhamini ili kupunguza njaa katika timu zetu hizi?

Hivi ni kweli wameshindwa kupata wachezaji wanaotamba VPL kuwafanya wawe “Brand ambassadors”?

Afisa wa masoko hawahawa wamekosa kweli timu yakuifanya iwe official patner wao?

Leo Emmanuel Okwi ameteuliwa kuwa balozi wa Tulia Marathon Mbeya imekua habari kubwa, lakini jiulize mchezaji anaeongoza kwa mabao VPL inakuaje mpaka msimu unaelekea mwisho anapata kuwa balozi wa Tulia Marathon pekee? Ni kwamba haonekani au maafisa masoko wa kampuni zetu za Kitanzania, wanataka kutuambia mastar wetu wa VPL hawakubaliki katika jamii au hawana soko machoni mwa Watanzania wengi?

Mchezaji bora wa msimu uliopita Mohamed Hussein “ZimbweJr” sijui alifaidika na nini na ule uchezaji wake bora kwa hizi kampuni zetu za hapa Bongo. Unatamani umuonee ameanzaa msimu akiwa anavalishwa na kampuni fulani ya nguo, awe ni balozi wa benki fulani na pia awe anawakilisha kampuni fulani ya vinywaji baridi lakini wapi hakuna kitu.

Image result for Mohamed Hussein 'Zimbwe JR'

Kuna kampuni nyingi zenye ushindani zilizopo katika soko moja ambazo kila siku zinashindania kuongeza “market share” katika soko na kuwazidi wenzao.

Kuna industry nyingi tuu zilizoo katika ushindani wa halii ya juu kama za kibenki, kampuni za vinywaji baridi na vilevi, kampuni za bima, hospitali binafsi, kampuni za dawa za meno, kampuni za mawasiliano na nyingine nyingi zilizopo katika ushindani.

Kampuni zote hizo chini ya Afisa masoko wao wameamua kutafuta njia zingine kutangaza biashaara zao ili kufikika kwa wateja na kutuachia timu zetu na mastar wetu wa VPL njaa kali na mamilioni yao wakiwapa wengine.

Timu kama Kagera Sugar, Mtibwa Sugar na Tanzania Prisons zimeshiriki ligi kwa muda mrefu. Lakini pia zikiwa na uongozi makini bila kusikia migongano ya kimaslahi kwa viongozi lakini leo hii zinacheza zikiwa hazina mdhamini wala kampuni yoyote ambayo ni official partner wao.

Inasikitisha wakati mwingine na inakera star kahim Ajibu hana mkataba hata mmoja wakati Christiano Ronaldo ana udhamini na makampuni yasiopungua 30.

Angalau DTB Bank wao wana balozi wao Mbwana Samata na tunategemea angalau waongezeke wengine katika wachezaji wetu wanaocheza ligi ya ndani.

Kwa afisa masoko wa kampuni zetu za Kitanzania angalau mgeukie na huku kwenye mpira na kuutumia kama moja ya njia zenu za kukuza masoko. Angalau muwafikirie wachezaji wetu kuwa mabalozi wenu wa bidhaa zenu. Mjitaidi kuwafanya wachezaji wetu tuwaone kwenye matangazo yenu ya bidhaa na katika social media zenu.

 

Sambaza....