Sambaza....

Klabu ya Simba baada ya miaka 13 imeandika tena historia ya kushiriki hatua ya makudi ya klabu bingwa Africa baada ya kuziondoa Mbabane Swallors na Nkana rangers katika hatua za awali. Hii ni tija si kwa Simba pekee bali hata kwa Taifa kwa ujumla.

Wachezaji wa Simba waliingia katika michuano hii na lengo la kuivusha klabu yao mpaka hatua ya makundi huku wakichangizwa kwa kiasi kikubwa na maneno ya msemaji wao Hajji Manara na mashabiki wao, na kweli walifanikiwa katika hili.

Aishi Salum Manula kipa namba moja wa timu ya Taifa na klabu ya Simba sc alisimama langoni kwenye michezo yote minne katika hatua za awali mpaka akifanikiwa kuipeleka hatua ya makundi klabu ya Simba. Lakini katika michezo yote minne aliyosimama langoni amekua na kiwango cha kutatanisha kidogo.

Kwa kiasi kikubwa safu ya ushambuliaji ya Simba inafanya kazi yake vizuri mpaka sasa imeweza kufunga jumla ya mabao 11 katika michezo minne. Lakini si magoli tuu yanayoweza kuiweka Simba salama lakini pia uimara katika ulinzi.

Ili Simba iweze kuvuka hatua hii ngumu ya makundi na kwenda robo fainali inahitaji kiwango bora cha Aishi Manula. Manula kwa kipindi hiki amekua mtu muhimu sana, amekua ndie ufunguo wa Simba kuelekea robo fainali ya klabu bingwa Africa.

Manula amekua na makosa mengi yanayoigharimu Simba kiasi kwamba kuwatia wasiwasi mashabiki wa Simba kwa kiwango chake anachokionyesha. Manula anatakiwa kuimarisha kiwango chake na kufuta makosa yake ili kuiwezesha Simba kufuzu robo fainali.

Aishi Manula anatakiwa kuihakikishia Simba ipo salama katika eneo la ulinzi kwa kuitumia mikono yake vizuri na kupunguza makosa. Manula anatakiwa kufuta makosa haya ili afungue mlango wa robo fainali.

Makosa ya Aishi Manula:

Mechi nne magoli manne

Aishi manula amecheza michezo minne na kukubali kuruhusu mabao manne katika nyavu zake. Alifungwa goli moja katika mchezo dhidi Mbabane nyumbani, halafu akaruhusu tena magoli mawili jijini Kitwe dhidi Nkana kabla ya kukubali tena bao moja alilofungwa na Walter Bwalya uwanja wa Taifa.

Aishi Manula akiwa langoni dhidi ya Mbabane Swallows.

Magoli yote hayo aliyofungwa Manula amekua akielekezewa tuhuma za moja kwa moja kwa kuruhusu magoli kizembe yeye mwenyewe au kwa kushindwa kuwapanga mabeki wake.

Magoli ya mbali

Aishi manula amekua akifungwa magoli ya aina moja mara kwa mara huku ikionekana anashindwa kabisa kuzuia mashuti ya mbali “Long range efforts” kutoka kwa wapinzani.

Katika mchezo wa Kitwe alifungwa goli na Kampamba akiwa mbali kabisa nje ya box huku akionekana kuruka tuu kiushahidi bila kua na uhakika wa kuucheza mpira. Si hilo tuu hata katika VPL anafungwa magoli ya aina hiyo kama alivyofungwa na Awadh Juma katika mchezo dhidi ya Lyon.

Kupanga mabeki:

Manula ameonekana kua na mapumgufu kidogo katika kuwaelekeza walinzi wake jinsi ya kujipanga langoni mwao wakiwa wanashambuliwa. Katia mchezo wa marudiano dhidi ya Nkana Walter Bwalya alifunga goli jepesi kutokana na mabeki wa Simba kutokukaa eneo husika haswa Pascal wawa na Nicholaus Gyan.

Mara kwa mara katika michezo ya VPL Pascal Wawa ameonekana akimfokea Manula kutokana na makosa kama haya.

Pascal wawa akipambana na Walter Bwalya

Hana ushindani namba wa uhakika:

Deo Munishi amekua na kiwango cha kusikitisha hasa baada ya kuonyesha kiwango cha kusikitisha katika mchezo w FA dhidi ya Mashujaa hivyo kuzidi kumpa amani Aishi manula kua hakuna kipa wa kiwango chake Simba.

Pia Salim Ally amekua na uwezo mzuri sana langoni lakini kukosa uzoefu kunamfanya kocha wa Simba kuendelea kumuamini Manula pekee.


Sambaza....