Mabingwa Afrika

Al Ahly Yapewa Ruhusu ya Mashabiki Kuelekea Mchezo wa Mabingwa Afrika

Sambaza....

Mamlaka za nchini Misri zimekubali mashabiki 52,000 kuhudhuria katika mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa kati ya Al Ahly dhidi ya Raja Casablanca.

Ahly ambao walifanikiwa kuvuka katika hatua ya makundi kwa kuwafunga Al Hilal mabao matatu kwa sifuri katika mchezo wa mwisho na hivyo kufuzu wakiwa sawa kwa alama 10 lakini wao wakiwa na wastani wa matokeo mazuri dhidi ya Wasudani hao.

Mashetani Wekundu hao watawakaribisha vigogo kutoka Morocco Raja Casablanca kwenye mchezo wa kwanza katika dimba la Kimataifa la Cairo April 21 Jumamosi hii.

Cairo International Stadium

Kuelekea mchezo huo Mashetani hao wamepata nguvu zaidi baada ya kukubaliwa na mamlaka za nchini mwao kuruhusu kuingiza mashabiki 52,000 na kuujaza uwanja. Awali kulikua na katazo la mashabiki katika viwanja vya soka nchini Misri kutokana na sababu za kiusalama na kupelekea michezo mingi nchini huo kuhudhuriwa kwa idadi maalum ya mashabiki.

Ahly ambao waliwatoa mwaka jana Raja Casablanca katika hatua kama hii watarudiana tena katika mchezo wa pili April 28 na itakua haina maana kama watapoteza mchezo huo ama watapata ushindi mwembamba dhidi ya wababe hao wa Morocco. Mshindi katika mchezo huo atakutana na kati ya Esperence de Tunis ama JS Kabyele katika nusu fainali.

Sambaza....