Blog

Alexander-Arnold aondolewa kikosini England.

Sambaza....

Beki wa kulia wa timu ya soka ya Liverpool Trent Alexander-Arnold ameondolewa kwenye kikosi cha timu ya England baada ya kupata maumivu ya mgongo ambapo kwa mujibu wa taarifa ya England ni kuwa alifika kambini akiwa na maumivu hayo lakini juhudi za kumtibu kwa haraka ziligonga mwamba..

Arnold ambaye aliitwa kwenye kikosi cha England kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya kufuzu kwenye fainali ya mataifa Ulaya (Euro 2020 qualifiers) ameondolewa jana na hakuna mchezaji yoyote ambaye ameitwa kuziba nafasi yake.

England inajiandaa na michezo miwili muhimu ya kuwani nafasi hiyo ambapo Ijumaa watacheza na Jahmuri ya Cheki siku ya Ijumaa kabla ya Jumatatu kukutana na Montenegro siku, na kutokana na kuwasili na maumivu hayo hakuwa na matumaini ya kucheza mchezo wowote kati ya hiyo.

Kwa sasa amerejea kwenye klabu yake ya Liverpool kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x