Yanga wakishangilia
ASFC

Alliance FC iliyo bora imetolewa na Yanga dhaifu.

Sambaza....

Jana kulikuwa na mchezo wa robo fainali katika uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza kati ya Alliance Schools na Yanga.

Katika mchezo huo ambao ulishuhudiwa timu hizi zikitoka sare ya goli moja kwa moja katika dakika za kawaida za mchezo.

Matokeo ambayo ilizipeleka hizi timu kwenda katika hatua ya mikwaju ya penati ambapo ilishuhudia Yanga wakiingia katika hatua ya nusu fainali kwa kuitoa Alliance Schools FC.

Baada ya mchezo huo afisa habari wa Alliance Schools FC amedai kuwa Alliance Schools FC bora imetolewa na Yanga dhaifu.

Akizungumza na mtandao huu wa Kandanda.co.tz Afisa habari huyo, Jackson Mwafulago amedai kuwa katika mchezo huo Yanga walikuwa dhaifu ukilinganisha na Alliance Schools FC.

Alizidi kusikitika kuwa wapenda soka wa Tanzania wataikosa timu bora katika michuano hii ya kombe la shirikisho.

Jackson Mwafulago ameomba msamaha kwa wapenda mpira kwa Alliance schools FC kutolewa kwenye michuano hii na kuahidi kuwa watajipanga vizuri kwa ajili ya michuano ijayo.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.