Sambaza....

Timu ya soka ya Alliance ya Jijini Mwanza imeonja kwa mara ya kwanza ushindi katika michezo ya ligi kuu toka ilipopanda baada ya kuichabanga timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) kwa mabao 2-1.

Mabao ya Dickson Ambundo na Juhudi Philimoni katika dakika ya tano na dakika ya 10 ndiyo yamepeleka furaha kunako kambi ya Alliance ikiwa wamecheza kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Bao pekee la KMC Katika mchezo huo limepatikana katika dakika ya 56 kupitia kwa nyota wa zamani wa Mbao FC ya jijini Mwanza, Mrundi Emmanuel Mvuyekule baada ya kuonganisha mpira wa mfulo na kumshinda kipa Ibrahim Isihaka wa Alliance.

Matokeo hayo yanawafanya Alliance kuchumpa hadi katika nafasi ya 19 wakiwashusha Mwadui FC mkiani baada ya kuzikamata alama 4 kibindoni katika michezo saba ambayo wameshacheza hadi hivi sasa huku KMC wakisalia katika nafasi ya 12 wakiwa na alama 7.

Sambaza....