Blog

Auusems kuendelea kuiongoza Simba SC

Sambaza....

Moja ya makocha wenye furaha wakati msimu wa Ligi Kuu ukiendelea ukingoni na Bingwa ameshafahamika, ni Mbeligiji, Patrick Auusems. Patrick ameiongoza kwa mafanikio makubwa klabu ya Simba SC, ikiwa pamoja na kufika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akiongea katika mkutano wake na waandishi wa habari, Muwekezaji mkuu wa klabu hiyo amemuhakikishia kazi kocha huyo, ikiwa pamoja na kumpa fungu kwaajili ya kusaini wachezaji kabambe.

Kocha ameshafikia malengo tuliyomuwekea tulikuwa tunataka ubingwa na kufika kwenye makundi ya Ligi ya Mabingwa, Mungu akitujalia kwenye wiki moja tutakaa nae tumuongeze mkataba … tutamueleza sehemu ambazo kuna mapungufu ili aendelee kufanyia kazi”- Mo Dewji

Kwa maelezo haya, ni dhahiri kabisa Aussems ataendelea kuongoza Mabingwa hao wa kibabe kabisa, ikiwa pamoja na kuzungumza naye mapungufu yake.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.