Ligi Kuu

Azam FC yamfukuzisha kazi Bakari Shime

Sambaza....

Klabu ya JKT Tanzania imemfukuza kazi aliyekuwa kocha mkuu wa klabu hiyo , kocha Bakari Shime “Mchawi mweusi”.

Kocha huyo ambaye aliipandisha timu kutoka ligi daraja la kwanza mpaka ligi kuu msimu huu amefukuzwa kazi baada ya timu yake kufungwa goli 6-1 dhidi ya Azam FC.

Matokeo haya yamechangia kwa kiasi kikubwa kwa uongozi wa JKT Tanzania kumfukuza kazi Bakari Shime.

Bakari Shime ” Mchawi Mweusi” amewahi pia kuwa benchi la ufundi la timu ya soka ya vijana iliyo chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys, msimu Jana kwenye michuano ya Afcon iliyofanyika nchini Gabon.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.