Uhamisho

Baada ya kutemwa Yanga, Juma Balinya asajiliwa timu kubwa!

Sambaza....

Mwanzoni mwa msimu huu Yanga walimsajili aliyewahi kuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya Uganda 2018/2019 akiwa na timu ya Police ya Uganda , Juma Balinya.

Juma Balinya alikuja kuziba nafasi ya mshambuliaji Makambo ambaye alisajiliwa na timu ya Horoya ya nchini Guinea lakini Juma Balinya hakufanikiwa  kufanya vizuri.

Balinya (Kulia)

Yanga waliamua kuvunja mkataba mwezi wa 12 mwanzoni mwaka jana hivo yeye kuwa mchezaji huru tena na siyo mchezaji wa Yanga.

Imeripotiwa Leo kuwa klabu kubwa nchini Kenya na Afrika Mashariki GorMahia imemsajili Juma Balinya na kuwa mchezaji rasmi wa timu hiyo.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.