Mabingwa Afrika

Baada ya Simba kufuzu, mchezaji Simba sc aweka rekodi ya kutisha

Sambaza....

Bao la Claotus Chota Chama la dakika ya 89 lililowavusha  “Wekundu wa Msimbazi” Simba mpaka hatua ya robo fainali katika Klabu Bingwa Africa limekuja na rekodi muhimu katika klabu hiyo kwa baadhi ya wachezaji.

Kinda wa Simba sc Rashid Juma amefanikiwa kuandika rekodi ya maana kwake baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya robo fainali na klabu yake ya Simba sc.
Rashid Juma anakua moja ya wachezaji wenye umri mdogo kabisa kuweza kuhusika kuivusha klabu yake hatua ya makundi na kufika robo fainali.

 

Rashid Juma akiwa na umri wa miaka 19 alicheza katika dakika chache katika mchezo dhidi ya AS Vita akiingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya James Kotei. Rashid Juma pia anakwenda kuandika rekodi nyingine ya kuwa miongoni mwa wachezaji wa Tanzania mwenye umri mdogo aliejumuishwa katika kucheza michuano mikubwa kabisa kwa ngazi ya Klabu barani Afrika katika hatua ya robo fainali.

Rashid Juma pia amejumuishwa katika kikosi cha Ngorongoro Heroes kitakachoivaa Eritrea katika mchezo wa kirafiki.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.