Uhamisho

Bandari FC yawabania Yanga mrithi wa Kindoki

Sambaza kwa marafiki....

Kuna habari ambazo zilikuwa zimeenea kuwa Golikipa wa Bandari FC Faruk Shikhalo amesaini Yanga, lakini jana timu ya Bandari FC imetoa taarifa rasmi kuwa bado hajasajili na Yanga.

Kwenye taarifa hiyo ya timu ya Bandari FC inadai kuwa Bandari FC inampango wa kuendelea na wachezaji wao muhimu wote na kutowaruhusu kwenda popote.

Kocha mkuu wa Bandari FC, Bernard Mwalala ambaye pia ni mshambuliaji wa zamani wa Yanga amedai kuwa mchezaji bado yuko na timu yao.

Faruk Shikalo (Katikati)

” Faruk Shikhalo bado yuko kwenye majukumu ya mechi za klabu zilizobaki na mkataba wake na klabu hiyo na yuko na furaha kuutumikia mkataba wake”.

“Mkurugenzi mtendaji wetu bwana Edward Odour ameniambia kuwa mpaka sasa hajapokea barua yoyote ile kutoka kwenye klabu yoyote ile ya kumtaka Faruk”.

” Kwa hiyo Faruk ni mchezaji wetu na anamkataba wetu hivo tutamchukulia hatua yoyote yule anayesambaza habari hizi za uongo kuhusu Faruk kusajiliwa Yanga”- ilidai taarifa hiyo ramsi kutoka klabu ya Bandari FC.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.