Ligi

Benfica ‘wamkata maini’ Jose Mourihno.

Sambaza....

Tetesi za kocha Jose Mourinho kupata kibarua majuma machache baada ya kufukuzwa kazi na Manchester United zimezimwa kwa aina yake baada ya klabu ya Benfica ambayo ndiyo alikuwa akihusishwa kujiunga nayo kukataa kuhusika na mazungumzo na kocha huyo anayesifika kwa soka la kujilinda.

Taarifa kutoka nchini Ureno zimesema kwamba licha ya Benfica kuhitaji kocha mwenye uzoefu baada ya kumtimua kazi Rui Vitoria juma lililopita lakini Jose Mourihno hayupo katika majina machache yaliyoorodheshwa kurithi kiti hicho.

Wababe hao wa Primeira Liga walimfuta kazi Vitoria ambaye amedumu klabuni hapo kwa miaka mitatu na nusu na kuisaidia klabu hiyo kutwaa mataji mawili ya ligi, lakini msimu huu ulikuwa mchungu na kushindwa kuhimiri mikimiki ya wapinzani wao FC Porto.

Mourinho ambaye alianzia kazi ya Umeneja kwenye klabu hiyo ya Ureno kwa kuiongoza michezo 11 na kushinda michezo sita alikuwa akitajwa zaidi na vyombo vya habari vya Ureno kurithi nafasi hiyo hasa baada ya kuonekana akiwa na mtoto wake wakati timu za Vitoria de Setubal na Santa Clara zikiumana.

Mourinho alifutwa kazi katikati ya mwezi Disemba mwaka jana katika klabu ya Manchester United kutokana na timu hiyo kuandikisha matokeo mabovu toka kuanza kwa msimu wa 2018/2019.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.