Sambaza....

Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” inaendelea na maandalizi yake ya mchezo wa kuitafuta tiketi ya kufuzu Afcon 2019 dhidi ya Lesotho utakaochezwa Novemba 18,2018 Maseru,Lesotho.
Katika mazoezi hayo golikipa Beno Kakolanya na mshambuliaji Yahya Zayd walipumzishwa baada ya kugongana,taarifa ya madaktari wachezaji hao wataendelea na mazoezi kuanzia kesho.
Wachezaji wanaocheza nje wataanza kuripoti kambini Jumapili Novemba 11,2018.
Wanaotarajiwa kuanza kuripoti ni Ramadhan Kessy(Nkamia,Zambia),Himid Mao (Petrojet,Misri),Rashid Mandawa(BDF,Botswana) na Abdi Banda (Baroka,Afrika Kusini).
Waliobaki wataripoti kuanzia Novemba 12,2018.

Sambaza....