Ligi Kuu

Bernard Morrison siyo muhimu -Bumbuli

Sambaza....

Sakata la Bernard Morrison na klabu ya Yanga linazidi kupamba kila uchwao , leo hii Afisa habari wa Yanga , Hassan Bumbuli amedai kuwa Bernard Morrison aliikuta Yanga ikiwa kubwa.

Afisa habari huyo wa Yanga bwana Hassan Bumbuli amedai kuwa Bernard Morrison aliikuta Yanga ikiwa na vikombe 27, kwa hiyo awepo au asiwepo Yanga itabeba ubingwa tu hata bila yeye.

“Bernard Morrison hata kabla hajaja Yanga , tulikuwa tumeshabeba ubingwa mara 27, tumeitwa mabingwa wa kihistoria kabla hata yeye hajaja , kwa hiyo uwepo wake hauizui Yanga”- alisema Afisa habari huyo.

Hassan Bumbuli alizidi kusema kuwa watu hawatakiwi kukuza suala la Bernard Morrison kama wanavyolikuza kwa sababu ni mchezaji tu kama walivyo wachezaji wengine.

“Kabla hajaja Yanga tulikuwa tumeshinda mechi nyingi sana za mzunguko wa kwanza , kacheza mechi tisa tu , nadhani watu wasilikuze sana hili suala “- alizidi kusema Hassan Bumbuli.

Kuhusu uwezekano wa Bernard Morrison kucheza kwenye mechi ya kombe la shirikisho yani Azam Federation Cup, Hassan Bumbuli alisema inategemeana na kocha atakavyomuona kama ana utimamu wa kimazoezi.

“Kwa kifupi wachezaji wengi wako sawa, tunasubiri mechi ya FA, kama kocha ataona Bernard Morrison yuko na match fitness basi atacheza mechi hiyo”- alisema Afisa habari huyo


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.