Bocco
Mabingwa Afrika

Bocco kuendelea kupiga penalti za Simba

Sambaza kwa marafiki....

Kocha mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema kuwa John Bocco ataendelea kuwa chaguo la kwanza la upigaji penalti kwenye timu hiyo.

Kocha huyo amedai kuwa hakuna kilichoharibika au kubadilika baada ya John Bocco kukosa penalti kwenye mchezo wa TP Mazembe uliofangika hapa Dar es Salaam , Tanzania.

Akizungumza na mtandao huu kwenye mazoezi ya mwisho kuelekea kwenye mechi ya marudiano ya mechi hiyo itakayofanyika Lubumbashi , amedai kuwa hawezi kubadilisha mpiga penalti.

 

John Bocco ataendelea kuwa mpiga penalti. Patrick Aussems amedai kuwa kilichotokea hapa Tanzania kwa John Bocco kukosa Penalti ni jambo la kawaida.

Amedai kuwa ni jambo ambalo linaweza kutokea popote kwa mchezaji yoyote kupoteza penalti hivo haliwezi kubadilisha kwa John Bocco kupiga penalti.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.