Carlinho
Blog

Carlinhos na sura yenye manufaa kwa Yanga

Sambaza....

Baada ya Tuisila, Mukoko, Sarpong, Yacouba, na nyota wengine kibao jana Yanga wamemtambulisha kiungo mshambuliaji Carlinhos kuwa rasmi ni mwananchi.

Anaitwa Carlos Sténio Fernandes Guimarães do Carmo, hio Carlos ndio inatamkwa ‘Carlinhos’ kunywa maji kwanza hapo usijing’ate ulimi.

Ni raia wa Angola mwenye umri wa miaka 25, kiungo wa mpira anacheza dimba la kati, pembeni na hata nyuma ya mshambuliaji wa kati kwa uwezo mkubwa.

Carlinho

Binafsi nawapangeza Yanga kwa kufanikisha usajili wake kwani ni mchezaji atakayeinufaisha timu hio katika nyanja mbali mbali ikiwemo hizi tatu.

Mosi ni uwanjani, hapa moja kwa moja nazungumzia uchezaji na kiwango chake ambapo kupitia baadhi ya video zake zinamuonesha anauwezo mkubwa kiuchezaji na kama ikisalia hivyo basi wananchi watapata burudani isiyo na kifani huku akichagiza ushindi na mafanikio ya timu kwa ujumla.

Pili ni biashara, hapa kubali ama kataa Yanga wamepata biashara inayojiuza kwa maana ya muonekano wa Carlinhos ni dhahiri kuwa anavutia kutizama hivyo kwenye mambo kama kutangaza jezi na biashara nyingine za klabu atawafaa sana wananchi na watanufaika kwa hilo.

Tatu, ni kukuza chapa ya Yanga, kwa fikra ndogo saana za upande hasi unaweza kuwabeza mashabiki wa Yanga wanaokwenda uwanja wa ndege kuwapokea wachezaji wao, lakini kwa jicho la tatu lazima utaona faida kuu kwa Yanga. Jana nyomi lilikua kubwa kuanzia pale uwanja wa ndege mpaka jangwani na sio bongo tu hata huko Angola alikotoka watu wamepigwa na butwaa kuona kijana wao akipokelewa kwa mapokezi makubwa namna ile.

Hii itakuza chapa ya Yanga kwa kiasi kikubwa watu wataitambua ni timu ya aina gani, wachezaji wengi watatamani kuja jangwani wapokelewe kama Carlinhos, Timu tofauti zitatamani kuja kucheza bongo na hili litaongezwa motisha na tamasha lao la wiki ya mwananchi.

Hongera saana Yanga, zingatieni biashara na mifumo yake.  Mwisho, hapa wanufaika hawatakua Yanga pekee bali ni soka la Tanzania kwa ujumla.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.