Chama akipiga mpira
Ligi Kuu

Chama, Okwi na Manula kuikosa Mbao.

Sambaza....


Leo hii kutakuwepo na mchezo kati ya Simba FC na Mbao FC utakaochezwa katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Simba imeamua kuutumia uwanja wa Jamhuri Morogoro kama uwanja wao wa nyumbani katika michuano ya ligi kuu baada ya uwanja wa Taifa kufungwa kwa ajili ya kufanyiwa marekebisho kwa ajili ya Afcon ya vijana.

Akizungumza kuelekea katika mchezo huo, kocha mkuu wa Simba, Patrick Assumes amedhitisha kuwa Simba itamkosa kipa wao namba moja Aishi Manula.

Aishi Manula aliumia akiwa na timu ya taifa. Pia Kocha Patrick Assumes amedhibitisha kuwa Kiungo mahiri wa timu hiyo Chama atakosekana katika mchezo huo.

Pia mshambuliaji wa Uganda , Emmanuel Okwi atakosekana katika mchezo huu wa Leo. Hii itakuwa pigo kwa Simba kwa kuwakosa wachezaji wao watatu ambao ni nyota ndani ya kikosi hicho.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.